Header Ads

Ester Kiama adaiwa kufulia

Staa wa filamu za Kibongo, Ester Kiama.
Staa wa filamu za Kibongo, Ester Kiama amedaiwa kufulia na ndiyo maana amekuwa haonekani kwenye viwanja vya kula bata kama ilivyokuwa kawaida yake.
Shosti wa karibu wa staa huyo aliyeomba jina lake lisitajwe alimwaga ubuyu kuwa,  Ester kwa sasa anapitia kipindi kigumu cha kuchalala, ndiyo maana zile vurugu zake za mjini zimeisha.
“Kafulia ile mbaya, hata ile staili ya kubadili magari imekwisha, viwanja ndiyo haonekani kabisa,” alidai mtoa habari huyo.

Alipotafutwa Ester kujibu madai hayo alisema kwa kifupi: “Jamani sijafulia, maisha siyo kujirusha kila siku wala kubadili magari, nafanya mambo yangu yenye manufaa.”

No comments