Header Ads

Gerald Hando, Paul James waachana na Clouds FM

 Dar es Salaam.
Watangazaji wawili wa kipindi maarufu cha Power Breakfast kinachorushwa na Clouds FM wameachana na redio hiyo, Mwananchi imetaarifiwa.
 

Watangazaji hao, Gerald Hando na Paul James, maarufu kwa jina la PJ, hawakushiriki kwenye kipindi cha jana asubuhi na Mwananchi ilithibitishiwa baadaye kuwa wamemaliza mikataba yao na uongozi wa kituo hicho hauna mpango wa kuwabakiza.
 

Awali, habari zilienea kuwa wawili hao wamefukuzwa kazi kutokana na matatizo ya kinidhamu. Lakini alipoulizwa kuhusu suala hilo, Hando alijibu: “Sijafukuzwa kazi hata kidogo, wala sijaacha kazi. Ninachofahamu mimi ni mfanyakazi wa Clouds Redio na leo (jana) sikusikika kwenye kipindi kwa sababu nilikuwa na udhuru.”
Uongozi wa Clouds unatarajia kutoa taarifa rasmi leo asubuhi kwenye kipindi cha Power Breakfast.


CHANZO; MWANANCHI 

No comments