• Latest News

  March 28, 2016

  Hatimaye! Riyama Ally amelipiwa mahari na mpenzi wake ‘sharobaro’

  Hatimaye! Taarifa ikufikie kwamba, staa wa kitambo wa Bongo Muvi, Riyama Ally amelipiwa mahari na mpenzi wake ‘sharobaro’ ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Haji  Mwalimu ‘Leo Mysterio’ huku mipango kabambe ya ndoa ikiendelea.
   
  Riyama ameliambia Wikienda kuwa, anamshukuru Mungu kumpata mtu anayeona ndiye anamfaa katika maisha yake na tayari sasa ni mchumba rasmi wa mtu, tena kijana anayempenda kwa dhati.
  “Sasa hapa ndiyo nimefika kwa kuwa nimekutana na mtu mwenye mapenzi ya kweli kwangu. Pia nafsi zetu zimeendana, hapa namuomba Mungu anyooshe mambo yaende kama vile tulivyopanga,” alisema Riyama ambaye amekuwa ‘singo’ kwa muda mrefu.
   1
  Kwa upande wake, Mysterio alisema kuwa anaamini safari yake ya muda mrefu imefika kwa kuwa amempata mwanamke anayempenda kutoka ndani ya uvungu wa moyo wake na kwa upande wake taratibu zote za uchumba amemaliza, anasubiri ndoa watakayofunga hivi karibuni.
   Stori:  Imelda Mtema, Wikienda
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Hatimaye! Riyama Ally amelipiwa mahari na mpenzi wake ‘sharobaro’ Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top