Header Ads

Joanitha, Gigy kuchuana kwenye uigizajiJoanitacut561.jpg
Fatuma Makame ‘Joanitha


Staa wa Filamu Bongo, Fatuma Makame ‘Joanitha’ na Video Queen Gift Stanford  ‘Gigy Money’ wanatarajia kuchuana kwenye filamu watakayocheza pamoja hivi karibuni baada ya Gigy kuchukuliwa na Kampuni ya Hamadombe kwa majaribio.
Akizungumza na Ijumaa, Joanitha ambaye ni bosi wa kampuni hiyo alisema wamebaini Gigy anao uwezo mzuri wa kuigiza lakini hajapewa nafasi hivyo wameona wakati anaendelea na U-Video Queen wake pia acheze filamu.
Gift Stanford  ‘Gigy Money’
“Unajua kwa sasa tumeamua kuwachukua wasanii kama ‘brand’ ili kushindana na makampuni mengine kwenye uigizaji hivyo tumemchukua Gigy Money na Tiko Hassan ambao wataingia kambini muda si mrefu,” alisema Joanitha.

No comments