Header Ads

Johari, Baba Haji wabambwa usiku mnene!

 Wakishutuka baada ya kupigwa picha.

 Walianza hivi.

Dar es Salaam: Mh! Mastaa wawili wa Bongo Muvi, Super Woman, Blandina Chagula ‘Johari’ na mwenzake, Adam Haji ‘Baba Haji’ wamebambwa wakiwa wamegandana kwa dakika kadhaa kwa madai ya ‘kumisiana’ kwa muda mrefu.
Ishu hiyo iliyopigwa chabo na paparazi wetu ilijiri usiku mnene kwenye Hoteli ya Rodizio iliyopo Masaki jijini Dar kulikokuwa na shughuli iliyoandaliwa na mastaa wa Bongo Muvi ya kumpongeza Paul Makonda kwa kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar na Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Baada ya kukutana, wawili hao walikumbatiana kwa dakika kadhaa kisha kila mmoja ‘alijibebisha’ kwa mwenzake huku wakinong’ona na kutoa vicheko vilivyowafanya mastaa wenzao kuwageukia na kuibua gumzo.
“Jamani kulikoni Johari leo kaja kwenye shughuli? Siyo kawaida yake na hivi anavyogandana na Baba Haji kila mtu anamkodolea macho,” alisikika mmoja wa wasanii chipukizi wa filamu.

Hata hivyo, Johari alipoona mwaga wa kamera ya gazeti hili unammulika yeye na Baba Haji alishtuka na kupiga mkwara kuwa hicho ndicho huwa kinamfanya anashindwa kwenda kwenye shughuli za mastaa.

“Sasa…(anamtaja paparazi wetu), picha zote hizo za nini? Kwanza ninyi ndiyo mnanifanya nisiwe nahudhuria kwenye matukio ya mastaa,” alisema Johari huku Baba Haji akiishia kucheka kisha wakatengana wakati wa kupiga picha na Makonda.
Shughuli hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibao ilimalizika mishale mibaya huku Johari na Baba Haji kila mmoja akitimua kivyake.


CHANZO: GPL

No comments