• Latest News

  March 30, 2016

  MISRI YAICHAPA NIGERIA 1-0, YAKWEA KILELENI KUNDI G


  Misri imekwea kileleni mwa Kundi G baada ya kuifunga Nigeria kwa bao 1-0 katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika.

  Katika mechi hiyo tamu iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Cairo, Misri imefikisha pointi 7 na kuweka matumaini ya kufuzu kwa asilimia 90 sasa.

  Nigeria inakuwa katika nafasi ya pili ikiwa na pointi mbili na Tanzania inashika nafasi ya mwisho ikiwa na pointi moja.


  Katika mechi ya leo, ushindani ulikuwa mkubwa na kila upande ulijitahidi ingawa wenyeji Misri walikuwa bora zaidi.

  Ramadhani Sobhy ndiye alikuwa shujaa baada ya kuifungia Misri bao katika dakika ya 65 baada ya shuti lake la chinichini kumbabatiza beki wa Nigeria na kumpoteza kipa kabla halijajaa wavuni.


  Nusura Nigeria isawazishe zikiwa zimebaki dakika tano baada ya shuti la Victor Moses kugonga mwamba na kurejea uwanjani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MISRI YAICHAPA NIGERIA 1-0, YAKWEA KILELENI KUNDI G Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top