Header Ads

Mkurugenzi wa Global Publishers alipofanya semina na wanafunzi wa Sekondari ya Benjamini jijini Dar es SalaamNILIPOFANYA SEMINA NA WANAFUNZI WA BENJAMIN SECONDARY SCHOOL-DAR
NILIPOFANYA SEMINA NA WANAFUNZI WA BENJAMIN SECONDARY SCHOOL-DAR Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kurudi kwa mara ya pili katika Shule ya Sekondari ya Benjamini jijini Dar es Salaam kuzungumza na wanafunzi kuhusu masomo na maisha yao.Nilifarijika sana kuwaona, ni kweli wanapitia katika kipindi ambacho wanahitaji faraja, kutiwa nguvu ya kusonga mbele zaidi.Ili kumsaidia mtu, si vizuri ukimpa fedha, mpatie kitu ambacho kitamfanya kupata fedha. Nilifarijika kuwaona, nyuso zao zilionyesha ushindi mkubwa, niliwaona madaktari, wanasheria, mawaziri wa baadaye shuleni hapo.Naamini kwa maneno niliyozungumza, yatakuwa mbegu katika maisha yao yote. Mbali na kumshukuru Mungu, pia naushukuru uongozi wa shule hiyo hasa kwa mwalimu mkuu, S.G Lugano kwa kunipa nafasi hiyo kubwa kuzungumza na wanafunzi hao.Pia nawashukuru kundi la wanafunzi linalojishughulisha na Motivational Speaking, S.Y.B (Scan Your Brain) kwa kunialika kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo. Namshukuru mwanafunzi na rafiki yangu, Buliba Magambo kwa kuhakikisha nafika shuleni hapo.Sina cha kuwapa katika nafasi mliyonipa, namuomba Mungu awaongoze na kuwalinda wote.
Posted by Eric Shigongo on Tuesday, March 8, 2016

No comments