• Latest News

  March 17, 2016

  Mwasiti ajitetea kufulia kimuziki

  STAA Mkongwe wa Bongo Fleva kutoka Jumba la Kuibua Vipaji vya Kuimba (THT), Mwasiti Almasi amefungukia maisha yake kimuziki kwamba hajafulia kwani kazi zake bado zinaendelea kuchezwa hasa mikoani.

  Akichonga na Showbiz Xtra Mwasiti anayebamba na Ngoma ya Sema Naye alisema, mashabiki wameshazoea kumuona akiimba muziki wa aina moja na katika wimbo wake mpya huo amebadilika na ndiyo chanzo cha wengi kutompokea vema.

  “Bado nafanya muziki na kwa sasa nina Wimbo wa Sema Naye japokuwa kwa hapa Dar ni kweli haujapokelewa vizuri lakini mikoani unachezwa sana tu,” alisema Mwasiti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Mwasiti ajitetea kufulia kimuziki Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top