• Latest News

  March 18, 2016

  Najma amtia uchizi wa mahaba Baraka da Prince, amdatisha kimapenzi!

   Baraka da Prince akiwa na Mwanadada Najma Dattan aliyewahi kutoka kimapenzi na Mr Blue na Diamond.
   
  Siyo siri tena! Mwanadada Najma Dattan aliyewahi kutoka kimapenzi na Mr Blue na Diamond, kafa kaoza kwa dogo anayefanya poa kwa sasa kwenye gemu la muziki, Baraka da Prince.
   
  Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya mapenzi wamebaini Baraka katiwa uchizi na mwanadada huyo shombeshombe kiasi kwamba kila wakati anatupia picha romantic akiwa na laazizi wake huyo.
  Unajua mshkaji anasemaje kuhusiana na penzi lake kwa mdada huyo? Hebu msikie: “Kusema ukweli huyo ndiye shemeji yenu, sina maneno zaidi ya hayo.

   
  Kanitia uchizi, kanidatisha, hilo ni juu yangu.”
  Kabla ya kuwa na Najma, Baraka aliwahi kudaiwa kutoka na Masogange na Nisha, mazingira yaliyotafsiriwa kuwa, msanii huyo ni mkali kwa totoz. Kwa jina lingine na yeye ni sukari ya warembo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Najma amtia uchizi wa mahaba Baraka da Prince, amdatisha kimapenzi! Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top