Header Ads

Penny azimia baada ya gari lake kupigwa mzinga maeneo ya Mikocheni jijini Dar!


Dar es Salaam: Bidada yamemkuta! Mtangazaji wa Zuku TV, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ amekumbwa na mkasa mwingine baada ya gari lake kupigwa mzinga maeneo ya Mikocheni jijini Dar, kwa kile kinachodaiwa alizimia barabarani kutokana na tatizo la ini linalomsumbua kwa sasa.

Chanzo makini ambacho kilishuhudia tukio hilo kilisema kuwa staa huyo alikuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota Mark X kwa mwendo wa kawaida lakini akaanza kupunguza spidi taratatibu kutokana na maumivu yaliyompata ghafla na kusababisha bodaboda kugonga gari lake kwa nyuma.
peni2Mpashaji wetu aliendelea kusema kuwa, wakati tukio hilo linatokea ilikuwa mchana kweupe bodaboda nusura wamfanyizie.
 peni3
Pamoja na watu kusogelea kwenye tukio, Penny aliendelea kukaa ndani ya gari akiwa amejilaza hadi alipopata nafuu ndipo akaanza kuondoa gari taratibu.
Wikienda lilipozungumza na Penny alisema alipatwa na hali hiyo huku mwili ukiishiwa nguvu lakini kwa sasa yuko sawa.

pennyPenny anakabiliwa na tatizo la kuharibika kwa ini kufuatia unywaji wa pombe kali kwa muda mrefu.
Hivi karibuni, Penny aliyekuwa mpenzi wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aliripotiwa kuwa na tatizo la ini kutokana na unywaji wa pombe kali.

 
Stori:  Imelda Mtema, Wikienda

No comments