Header Ads

SABABU YA CHAD, TAIFA STARS SASA KUBAKI NA POINTI MOJA TU

Kujitoa kwa Chad katika mechi za kuwania kucheza Afcon wala si jambo jema.

Kwa hali ilivyo, kila timu italazimika kudondosha pointi moja kutoka katika Kundi G iliyopo Stars.

Hivyo, Stars yenye pointi 4, itabaki na pointi moja tu, Nigeria itabaki na pointi mbili huku Misri ikibaki kileleni na pointi tano.

Jambo hilo linapoteza kabisa matumaini ya Taifa Stars huku ikiacha matumaini makubwa kabisa kwa Misri hasa kama itashinda mechi yake dhidi ya Nigeria, keshokutwa.


Kama Misri itashinda, basi itakuwa imefuzu kucheza Afcon kwa asilimia 95.

Tayari Stars ilikuwa imecheza mechi tatu, ilianza kwa kupoteza dhidi ya Misri ugenini, ikatoka sare ya bila mabao na Nigeia jijini Dar es Salaam kabla ya kushinda kwa bao 1-0 mjini ND'jamena dhidi ya wenyeji Chad ambao wamejitoa kwa madai hawana nauli.

No comments