Header Ads

Vee Money: Nachukia kuitwa mwanamuziki wa kikeStaa wa Ngoma ya Niroge, Vannessa Mdee ‘Vee Money’ kwa mara ya kwanza amefungukia kuchukizwa na baadhi ya watu wanaomwita mwanamuziki wa kike.

Akichonga katika kipindi cha Exclusive kinachorushwa na Global TV Online, Vee Money alisema kuwa angependa kufananishwa na wanamuziki wengine wote na siyo kutengwa kwa kuwa mwanamke basi atambulike kama mwanamuziki wa kike.

“Sawa naapenda muziki lakini kinachoniuzi mara nyingi ni kutofautishwa na kuchukuliwa kama mwanamuziki wa kike. Napenda kuujulikana kama mwanamuziki inatosha,” alisema Vee Money.

Vannessa amezungumza mengi yanayomuhusu yeye na maisha. alifanya mahojiano hayo kisha na kupiga picha na baadhi ya wafanyakazi wa global publishers. Mahojiano kamili yanapatikana keshokutwa Jumatatu kupitia www.globaltvtz.com

Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

No comments