Header Ads

VIDEO: Shuhudia Exclusive Interview ya Vanessa Mdee

Vanessa Mdee ‘Vee Money akiwa ndani ya Studio za Global TV Online Ijumaa iliyopita.
UKISHUKA katika Jiji la Lagos, Nigeria kisha ukaulizia miongoni mwa lebo kubwa za muziki ni wazi utatajiwa Chocolate City yenye vichwa hatari kama vile M.I, Ice Prince, Victoria Kimani na wengine kibao.
Victoria Kimani si Mnigeria bali ni Mkenya aliyeweza kutoboa kimataifa na sasa maisha yake kimuziki yapo nchini Nigeria. Mashabiki wengi hususan wa Kenya wana cha kujivunia kupitia Kimani kutokana na kuitambulisha nchi yao.
vanessa (3)-001
Kwa Tanzania tunaye mwanadada, Vanessa Mdee ‘Vee Money anayebamba kimataifa kupitia muziki. Vee Money aliyeanzia utangazaji kupitia Kituo cha MTV na Choice FM, kwa
mara ya kwanza alianza kusikika kwenye muziki kupitia Wimbo wa Me and You alioshirikiana na Ommy Dimpoz.
Kwa sasa bi’dada huyo anabamba na Ngoma ya Niroge iliyopikwa na Prodyuza Nahreel na kideo chake kuongozwa na Msauz, Justin Campos.
Mwishoni mwa wiki iliyopita Vee Money alitinga ndani ya Mjengo wa Global Publishers, Bamaga- Mwenge na kufanyiwa mahojiano ya moja kwa moja kupitia Kipindi
cha Exclusive kinachorushwa na Global TV Online na katika makala haya anafunguka zaidi;
vanessa
Over Ze Weekend: Nini kilikufanya ukaandika Wimbo wa Niroge?
Vee Money: Nilitaka kuonesha mapenzi ya dhati kwa kila mtu anayempenda mpenzi wake atatamani kuwa hivyo.
Over Ze Weekend: Na wimbo huo umeutunga wewe?
Vee Money: Hapana! Sehemu kubwa katunga rafiki wa mimi na mtunzi mahiri, Barnaba Boy na tuliutungia studio kwa Nahreel.
Over Ze Weekend: Inasemekana mna bifu kati yako na Shaa?
Vee Money: Bifu? Hapana!
Over Ze Weekend: Umekutana na mastaa wengi wa dunia, una mpango wowote wa kolabo nao?

No comments