Header Ads

Wapaka rangi wanavyomaliza kimapenzi wake za watu na Mastaa, Ripoti inatisha CHANZO: GAZETI LA IJUMAA - GLOBAL PUBLISHERS
Dar es Salaam: Vijana wanaofanya kazi ya kuwapaka rangi na kuwafanyia masaji za miguu wanawake, wamegandwa na skendo ya kutembea na wateja wao hao huku mazingira ya kazi yao yakitajwa kuwa chanzo, Ijumaa lina ripoti ya kutisha!

MAENEO YA SALUNI
Kwa muda mrefu, wanahabari wetu walifanya uchunguzi kwenye saluni mbalimbali jijini Dar katika maeneo ya Kinondoni, Mwenge, Sinza, Kariakoo na Posta ambapo ilibainika kuwa, vijana hao wakati mwingine wamekuwa wakishawishi au kushawishiwa na wateja wao kufanya nao mapenzi baada ya kuwapa huduma.
Wakizungumza na Ijumaa kwa sharti la kutotaka kupigwa picha, baadhi ya vijana wanaofanya kazi hiyo walisema kuwa, mazingira wanayofanyia kazi yamekuwa hatarishi kwao kwani wapo wanawake hasa wake za watu wanaowafanyia makusudi kwa kuvaa kihasara kisha kukaa kimitego wakati wanafanyiwa urembo huo.


“Kusema ukweli siyo wanawake wote wenye tabia ya kututega lakini baadhi yao ni shida. Unakuta mwanamke anakuja kwa nia ya kupaka rangi lakini nguo alizovaa, mmhh!
“Ukimpa kitaulo ili angalau ajifunike anakuambia acha, eti hataki kujibanabana. Akikaa sasa hayo mapozi yake, mara ajigeuze hivi mara vile. Mbaya zaidi baadhi yao hawavai makufuli (nguo ya ndani). Sasa kama ni mwanaume kweli uliyekamilika utaweza kuvumilia?” alihoji kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Saidi anayefanya kazi hiyo maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar.
 

Naye John Kihaso anayefanya kazi hiyo maeneo ya Magomeni alisema: “Hii kazi inahitaji uvumilivu sana, wanakuja wanawake wa kila aina hapa, wengine wakiwa na malengo yao. Kwa mfano juzi, tukiwa hapa tunapiga stori tuligundua kuna mama mmoja ambaye amekuwa akija kutengenezwa miguu ametembea na vijana wanne bila kujijua.
“Anavyovaa tu unajua huyu ana lake jambo, lakini mikao yake pia inaonesha hajijali na anataka kututega tu, matokeo yake sasa hawa wanawake wakikutana na vijana wapenda ngono, hawawaachi, wanatembea nao na ndiyo maana kweli ukifuatilia utagundua wapo wanawake wanaotembea na sisi.”

HATA MAJUMBANI NAKO
Akisimulia jinsi mchezo huo unavyokuwa, kijana mwingine anayefanya kazi hiyo kwa kutembea mtaani alisema, yeye amekuwa akipata zali la kuitwa majumbani kwa watu kuwapaka rangi wanawake lakini huko ndiko kwenye vishawishi zaidi.
“Mimi sina ofisi maalum ila huwa napata tenda maeneo mbalimbali, tatizo linakuja pale ambapo unakwenda nyumbani kwa mtu, unamkuta mwanamke peke yake, unamtengeneza miguu halafu ukimaliza anakuingizia mambo ya mapenzi, tena wakati mwingine anakuahidi kukulipa zaidi ndiyo maana wengi wetu tunajikuta kwenye mtego,” alisema kijana huyo.


MCHEZO UNAKUWAJE?
Kwa upande wake Ramso Juma, anayefanya kazi hiyo maeneo ya Manzese-Darajani alisema: “Iko hivi, unakuta mdada anakuja kwenye eneo lako la kazi, wakati unamtengeneza kucha anakuletea utani, mara kakukalia vibaya halafu anakutana na kijana ambaye ni ‘mzima’ kabisa.
“Kinachofuatia hapo kijana ataomba namba ya simu, baadaye anamtafuta. Acha hilo, anaweza kuja mwanamke kupakwa rangi au kutengenezwa miguu, wakati unaendelea na kazi yako anaanza kuonesha mihemko ya kimapenzi halafu yeye mwenyewe anadai eti umemtia majaribuni, kinachoendelea baada ya hapo ni nini sasa?” alihoji Ramso akimtaka mwandishi ‘kujaza mwenyewe’.


HATA MASTAA NAO
Aidha, uchunguzi huo ulibaini kwamba, ukiacha baadhi ya wake za watu kujirahisi kwa vijana hao, mastaa pia wamekuwa wahanga.
Kijana mmoja anayefanya kazi hiyo kwenye saluni moja iliyopo Kijitonyama alisema: “Hapa wanakuja mastaa wengi, lakini si unajua uvaaji wao, tena wengine hawavai makufuli, matokeo yake akija anakusababishia majaribu na kujikuta uzalendo unakushinda. Kama hatakuanza yeye basi unaweza kushangaa unaomba namba.”


SIYO WANAWAKE WOTE
Hata hivyo, wakizungumza na Ijumaa, baadhi ya wanawake ambao ni wateja wakubwa wa vijana hao walisema kuwa, mwanamke kutembea na wapaka rangi wanataka wenyewe kwani wapo wanaotengenezwa miguu yao katika mazingira yasiyo hatarishi na hakuna kinachoendelea.
“Unajua hizi tabia inategemea na mtu, wapo wanawake ambao wanajiheshimu, wanavaa nguo ndefu na huwa hawanaga utani na vijana hao. Ukiwalegezea lazima watakuchukulia poa,” alisema mama Julieth wa Sinza jijini Dar na kuongeza:
“Wengi ambao wanatembea na hawa vijana wanajiuza, anaenda kupaka rangi pale lakini akiingiziwa mambo ya mapenzi, hakatai. Pia wapo wanawake ambao hawajiheshimu halafu wana pepo wa ngono, hao ndiyo wanatufanya waume zetu watufikirie vibaya tunapokwenda kupakwa rangi.”


MSIKIE HUYU MSANII
Katika pitapita, waandishi wetu walimnasa msanii wa filamu Bongo, Brandy Godwin (Picha kubwa mbele) akipakwa rangi kwenye saluni moja iliyopo Kinondoni na alipoulizwa juu ya madai ya wanawake wakiwemo mastaa kutembea na vijana wapaka rangi alifunguka:
“Hayo mambo yapo sana lakini kiukweli inategemea na tabia ya mtu, mwanamke anayejiheshimu hawezi kufanya upuuzi huo. Kwa mfano, mimi nimekuja hapa kutengenezwa miguu, haijalishi nimevaaje lakini ‘so long’ najiheshimu, namheshimu mtu wangu, siwezi kujirahisi kwa vijana hawa.”


KUTOKA DAWATI LA IJUMAA
Kufuatia uchunguzi huo ambao unaonesha kuwepo kwa baadhi ya wanawake kutembea na vijana wapaka rangi, dawati la Ijumaa linashauri yafuatayo;
Kwanza, wanawake wanaokwenda kutengenezwa miguu, wasikubali kuoshwa hadi mapajani, wasijianike watupu, wavae kiheshima na kama kwa bahati mbaya umekwenda na nguo fupi, omba kitaulo ili kutomshawishi huyo anayekutengeneza.
Pili, vijana wanaofanya kazi hii wajue kwamba, kutembea na wanawake eti kisa wametegwa wakiwa kazini ni kujihatarishia maisha yao, pia kujipunguzia vipato kwani wanawake wengine wanakwenda kwa nia ya kuwachuna.
Tatu, wanaume wasiwakataze wapenzi wao kwenda kutengenezwa kucha kwa sababu ya ripoti hii, kikubwa ni mtu na mtu wake kuzungumza juu ya kujiheshimu na kuthamini mwili wake.
Ifahamike kwamba mwanamke kukaa mapaja wazi mbele ya mwanaume ni kujidhalilisha na kuchochea vitendo vya ngono.

Imeandikwa na Hamida Hassan, Gladness Mallya na Mayasa Mariwata

No comments