Header Ads

Wastara atoroshwa hospitalini kisha kupelekwa hoteli ya mafichoni huku akiendelea na matibabu


Morogoro: Taarifa mbaya! Staa wa Bongo Muvi, Wastara Juma ambaye mapema wiki iliyopita alidai kupewa talaka la mumewe, Sadifa Khamis Juma, Mbunge wa Donge, Zanzibar, anadaiwa kutoroshwa hospitalini kisha kupelekwa hoteli ya mafichoni huku akiendelea na matibabu.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Wastara aliyekuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Misheni ya St. Herry Health Center iliyopo mjini hapa, aliondolewa wodini hapa usiku mnene huku akiwa bado hali yake ya kiafya haijatengamaa tangu alipolazwa mapema wiki iliyopita akisumbuliwa na presha na kisukari na baadaye kupoteza fahamu.
 
WASTARA (3)
Wikienda lilifika hospitalini hapo Jumamosi iliyopita na kuthibitishiwa kuondolewa kwa msanii huyo na mtu aliyedai kuwa ni babu yake aliyetajwa kwa jina la Abdulaziz Babu.
Kwa mujibu wa mmoja wa wahudumu waliokuwa zamu walioomba hifadhi ya majina, jamaa huyo alidai kuwa Wastara aruhusiwe kwani alihofia usalama wake na kwamba sehemu aliyopanga kumpeleka ni salama zaidi.
 
WASTARA (2)
Baada ya kunusa ‘ubuyu’ huo hospitalini hapo, Wikienda lilimsaka Wastara kujua mahali alipo na hali yake lakini jitihada hizo ziligonga mwamba kwa kuwa namba yake ya simu haikuwa hewani.

Alipotafutwa mtu huyo anayedai ni babu wa Wastara alifunguka: “Ni kweli nimemuondoa Wastara hapo hospitalini kwa sababu za kiusalama. Yupo hotelini lakini siwezi kukuelekeza ni sehemu gani kwa sababu ukiandika itajulikana na tatizo litakuwa palepale.”
Wastara alikumbwa na hali hiyo ikidaiwa ilitokana na mgogoro wa ndoa yake na Sadifa iliyofungwa hivi karibuni na kushindwa kudumu.

 Stori:   Dustan Shekidele, Wikienda

No comments