• Latest News

  April 17, 2016

  AHLY WAPANGA KUIPELEKA YANGA NJE YA MJI WA CAIRO, YAELEZWA MECHI NI ALEXANDRIA


  Wakati Yanga inaondoka leo kwenda Cairo nchini Misri kuivaa Al Ahly, dalili zinaonyesha mechi hiyo lazima itachezwa kwenye mji wa Alexandria.

  Alexandria ni mji ulio kaskazini mwa nchi ya Misri na mwaka juzi Yanga walicheza kwenye uwanja wa jeshi wakati walipoivaa Al Ahly.

  Inaonekana bado hakuna usalama wa kutosha katikati ya jiji la Cairo, hivyo mechi hiyo inaweza kupelekwa Alexandria na sasa tayari ni asilimia 90 haitachezwa Cairo.

  "Hawasemi vizuri lakini taarifa tulizonazo kuwa mechi ni Alexandria na si Cairo. Hivyo watu wakija lazima watasafiri tena kwa takribani saa tatu hadi nne kwenda Alexandria," alisema Mtanzania anayeishi Cairo.

  "Unajua bado wana hofu ya usalama, ingawa kuna taarifa kwamba ile mechi dhidi ya Nigeria inawapa matumaini kuwa watu watatulia."

  Katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam, Yanga ilitoka sare ya bao 1-1, hivyo inalazimika kushinda au sare ya kuanzia mabao mawili na kuendelea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: AHLY WAPANGA KUIPELEKA YANGA NJE YA MJI WA CAIRO, YAELEZWA MECHI NI ALEXANDRIA Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top