Header Ads

Amanda Poshi ageuka gumzo makaburi

Staa wa Filamu Bongo, Amanda Posh.
Staa wa Filamu Bongo, Amanda Poshi hivi karibuni aligeuka kuwa gumzo kutokana na mwili wake kupungua tofauti na alivyokuwa zamani. Ishu hiyo ilitokea katika Makaburi ya Kinondoni, Dar wakati wa kumbukumbu ya marehemu Steven Kanumba ambapo mastaa walionekana kumshangaa na kujadili juu ya muonekano wake.

Baada ya kuona na kusikia jinsi wasanii na watu mbalimbali walivyokuwa wakimjadili, paparazi wetu alimfuata na kumuuliza kulikoni kupungua hivyo ambapo alisema; “Watu kunijadili na kunishangaa sijali ila naufurahia huu mwili kwani zamani nilikuwa nalazwa hospitali kila kukicha kwa tatizo la presha na lehemu ‘Cholesterol’ ilikuwa nyingi na daktari
alinishauri nipungue kwa sasa niko vizuri na kilicho-nifanya kupungua hivi ni mazoezi na kufanya ‘diet’ tu wala situmii dawa yoyote, hapa limebaki tumbo ndilo naendelea kulipunguza tena,” alisema Amanda.

No comments