• Latest News

  April 26, 2016

  Aunt Ezekiel adaiwa kumchepuka Iyobo

  Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amekwaa skendo ya kudaiwa kumsaliti mpenzi wake, Moses Iyobo na kuchepuka na jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Mula.

   Chanzo kilicho karibu na mwigizaji huyo kimevujisha ubuyu kuwa, Aunt amekuwa akimsaliti Iyobo kwa muda mrefu lakini amelifanya jambo hilo kuwa siri. 

  “Aunt mjanja amekuwa akichepuka lakini kwa siri sana, wanazurura katika viwanja mbalimbali na huyo jamaa lakini huwezi amini wanakuwa makini kweli hakuna mtu anayeweza kuwajua. “Wanahakikisha jamaa anakuwa na wenzake ili asiweze kujulikana kirahisi. 

  Ukiwaona wanakula bata unawaona kama ni kampani moja lakini wenyewe wanajua nini wanafanya,” kilisema chanzo chetu. 

  Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kilimtumia picha mwanahabari wetu zinazo muonesha Aunt akiwa na jamaa huyo katika pozi linaloashiria wana urafi ki uliopitiliza. 
   
  Baada ya kutumiwa picha hizo, mwanahabari wetu alimvutia waya Aunt ili aweze kuzungumzia ishu hiyo ambapo alipopatikana, alikiri kumfahamu Mula lakini akadai ni rafi ki yake wa kawaida, akiwashangaa watu wanaoeneza uvumi huo.

  “Hakuna kitu kama hicho. Huyo jamaa ni mshkaji tu, nimeona hata mimi kuna mdada ndiyo alianzisha huo uvumi Insta, anaeneza uongo tu.

   Huyo kaka ni mshkaji na hata Moze anamjua,” alisema Aunt. Jitihada za kumpata Mula ili aweze kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kutopatikana hewani
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Aunt Ezekiel adaiwa kumchepuka Iyobo Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top