• Latest News

  April 20, 2016

  AZAM TV YAFANYA KWELI, YAZINDUA KIWANDA CHA FILAMU

  AZAM TV kupitia chaneli yake ya Sinema Zetu, mapema leo imezindua rasmi ‘projekti’ iliyopewa jina la Kiwanda cha Filamu, na kipindi kipya kiitwacho Taxi,  vyenye lengo la kuibua vipaji vya wasanii wa maigizo  na wapiga picha za video chipukizi.

  Meneja Masoko na Mauzo wa Azam Media, Mgope Kiwanga, akifafanua zaidi namna projekti hiyo itakavyonufaisha watu wengi.
  Projekti hiyo ambayo ilianzishwa mwanzoni mwa Machi mwaka huu ilitoa furasa kwa watu mbalimbali ambao wangependa kushiriki kutuma kazi zao na wamepatikana zaidi ya washiriki 200.


  Akizungumza na wanahabari katika uzinduzi huo kwenye ofisi za Azam zilizoko eneo la Tazara jijini Dar, Msimamizi wa Uzalishaji wa Sinema Zetu, Zamaradi Nzowa, alisema washiriki hao watawachuja chini ya majaji akiwemo muigizaji wa siku nyingi hapa nchini, Suzan Lewis ‘Natasha’, ili kuwapata  washiriki 22.

  Baada ya kupatikana, watapatiwa mafunzo mafupi kisha wao pamoja na mastaa wa filamu hapa nchini watashiriki kwenye tamthilia itakayojulikana kwa jina la Taxi.

  Muigizaji Suzan Lewis ‘Natasha’, (kushoto) akimlisha keki msanii na mtangazaji mahari Bongo, Daniel Kijo.

  Nzowa alisema: “Washiriki ni kuanzia umri wa miaka 18 na kesho Jumatano pale Coco Beach ndipo tutaanza kufanya mchujo wa awali ambapo mpaka mwisho tunatarajia kupata waigizaji 20 na wapiga picha wawili ambao watashiriki kwenye tamthilia ya Taxi ambayo itazinduliwa Julai mwaka huu na itakuwa ikionyeshwa katika chaneli yetu ya Sinema Zetu.” 

  Mwandishi wa gazeti la Championi, Mohamed Mdose (kushoto) akilishwa keki na Natasha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: AZAM TV YAFANYA KWELI, YAZINDUA KIWANDA CHA FILAMU Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top