• Latest News

  April 24, 2016

  Breaking News: Mwanamuziki Nguli wa Congo Papa Wemba Afariki Dunia  Mwanamuziki nguli wa Congo Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia leo.

  Habari zilizotufikia hivi punde zinasema marehemu Papa Wemba amefia hospitali alikokimbizwa mara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu wakati akiwa katika onesho jukwaani.

  Papa Wemba alizaliwa June 14, 1949 huko Lubefu katika wilaya ya Sankuru nchini Congo. Alijipatia umaarufu sana kwa sauti nyororo na midundo ya Soukous ulimwenguni kote, ikiwamo Tanzania ambako amezuru mara kadhaa na kujizolea mashabiki wengi

  Papa Wemba  alipoanguka na kupoteza fahamu katikai ya onesho
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Breaking News: Mwanamuziki Nguli wa Congo Papa Wemba Afariki Dunia Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top