Header Ads

Clattenburg kuchezesha fainali ya Kombe la FA ...kati ya Man United v Crystal Palace, Mei 21


MWAMUZI Mark Clattenburg atachezesha mchezo wa fainali wa Kombe la FA.

Chama cha Soka cha England (FA) kimetangaza jana kwamba mwamuzi huyo ndio atachezesha mchezo huo wa fainali kati ya Manchester United na Crystal Palace utakaochezwa Mei 21 mwaka huu.

Clattenburg ambaye alichezesha mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Atletico Madrid, ambao walishinda bao 1-0 dhidi ya Bayern Munich juzi usiku.

“Nafikiri kila mwamuzi ambaye hajachezesha fainali hizi anafanya kazi kwa bidii ili achezeshe na ni fainali kubwa,” alisema Clattenburg.

Refa huyo amechezesha michezo 27 ya Ligi Kuu England msimu huu, akionyesha kadi za njano 81 na nyekundu sita.

No comments