Header Ads

Gardner alazimishwa kudansi laivu wimbo wa Jide!

Judith Wambura ‘Jide’.

Stori: Sifael Paul, Wikienda
Dar es Salaam: Noma sana! Mtangazaji anayetumikia Kituo cha Radio E-FM cha Dar, Gardner G Habash amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kulazimishwa kuserebuka wimbo mpya wa mtalaka wake, Judith Wambura ‘Jide’ unaoitwa Ndi Ndi Ndi.
Tukio hilo lilijiri juzikati ndani ya Ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama, Dar ambapo Gardner alikuwa MC wa shughuli ya bethidei za mastaa na watu wa kawaida waliozaliwa Machi.
Wakati shughuli ikiendelea huku watu wakikata keki na kufungua ‘shampeini’, ghafla DJ aliachia wimbo huo uliosababisha baadhi ya watu kupiga kelele wakitaka Gardner aucheze, jambo ambalo alilifanya kwa kunyong’onyea huku akirudi nyuma hadi msimamizi wa ukumbi huo alipomuomba DJ auondoe wimbo huo.

gardner (1)
 Mtangazaji anayetumikia Kituo cha Radio E-FM cha Dar, Gardner G Habash.

Hata hivyo, baada ya kubadilisha wimbo huo ambao inadaiwa Jide amemuimba Gardner, shughuli iliendelea kama kawa huku baadhi ya watu wakisema kuachana kwao si uadui kiasi cha kushindwa kucheza wimbo wake.
Wikienda lilipomtaka Gardner kuzungumzia ishu hiyo na kwamba wimbo huo ameimbwa yeye, hakuwa tayari. Kwa upande wake Jide alisema hajamuimba Gardner na kwa sasa hataki maswali yanayomhusu jamaa huyo ambaye walipeana talaka mapema mwaka huu baada ya kudumu kwenye ndoa kwa takriban miaka kumi.

No comments