Header Ads

Gerald Hando kuendelea kusikika asubuhi, lakini sio Clouds FM, ni redio pinzani!


Kupitia Instagram, Hando amedai kuwa ameacha kwa hiari yake baada ya mkataba wake kumalizika. Amedai kuwa ataendelea kusikika kwenye kipindi cha asubuhi lakini katika redio nyingine. Kuna uwezekano mkubwa akahamia EFM ambayo imewachukua watangazaji wengi wakongwe kutoka vituo vingine.

Hii ni taarifa yake:

Kwa Takribani Siku 3 Sasa Kumekuwa Na SINTOFAHAMU Na Kwa Baadhi Ya Ndugu Na Marafiki Imezua Taharuki Kuhusu Ajira Yangu Na Clouds FM..Naamiini Sasa Kwa Upande Wangu Ni Wakati MUAFAKA Kutoa TAMKO Rasmi Baada Ya kufuata Taratibu Zote Muhimu…KUANZIA LEO TAREHE 1 April 2016…Mimi Si Mfanyakazi Tena Wa Clouds Media Group Na Hii Ni Baada Ya Kwisha Rasmi Kwa Mkataba Wangu Na Clouds Media Group Jana 31 March 2016…Nimeamua Hivi Kwa HIARI Yangu Mwenyewe Bila SHINIKIZO Wala RABSHA Na Mwajiri Wangu Huyo Wa ZAMANI..Napenda Nikujulishe Tu Kuwa Nitaendelea Na Kazi Hii Hii Ya Utangazaji Ila Sasa Nitakua Na Kituo Kingine Na SI Clouds TENA…Wapi Na Lini Ni Suala La TIME…Jiandae Kuendelea Kufurahia ASUBUHI YAKO KATIKA FREQUENCY MPYA SOON. ..Haya Ni Masuala Ya FURSA…IKIJA UNAIKAMATA FASTA…Stay Cool…Stay Tuned

No comments