Header Ads

Gigy amjia juu Lulu Ladiva

VIDEO Queen Gift Stanford ‘Gigy Money’ amemjia juu mwenzake Lulu Abbasi ‘Lulu Ladiva’ kwa kauli yake kuwa hakuna muuza sura yoyote Bongo anayemfikia kimvuto na thamani kubwa kikazi.


Lulu Abbasi ‘Lulu Ladiva’

Akipiga stori na paparazi wetu, Gigy Money alisema, anamshangaa mwanadada huyo kwani hana lolote la maana zaidi ya kupenda kujisifu, kwani hamgusi kwa chochote, siyo kwa mvuto wala figa bomba aliyonayo. “Ana nini huyo, tena ananifanya nizidi kumchukia, kwa kipi hasa alichonacho, asithubutu kuropoka tena huo ujinga wake na asisogee kwenye 18 zangu, asijilinganishe na mimi,” alisema.


No comments