Header Ads

KABLA SIJAFA LAZIMA DUNIA INISAMEHE-2


Upelelezi wa maaskari wa shirika la kijasusi la Marekani FBI ulifanyika karibu maeneo yote yaliyozunguka jengo la WTC, gari la tajiri David Syndrome lilikutwa eneo lile, maaskari walilitambua kwa namba zake, lilikuwa ni miongoni mwa magari yaliyopekuliwa vibaya, maaskari waligutuka walipokiona kikaratasi kilichoandikwa maneno ya ajabu ndani ya gari hilo.
“I’m very sorry to the people in the world, I’m asking for their forgiveness that I can be forgiven also in heaven, because I have killed so many innocent people! Please forgive me all the people in the world!”(Naomba samahani kwa nyinyi watu wote duniani ninaomba msamaha wenu ili niweze kusamehewa mbinguni kwa sababu nimeua watu wengi sana wasio na hatia, tafadhali nisameheni!)
Kikaratasi kile kiliwashtua sana FBI walishindwa kuelewa kama ni kweli mfanyabiashara huyo aliyeipenda Marekani ndiye aliyekuwa amefanya ukatili wa kulipua jengo hilo.
“How comes an American do this to his own country!”(Inawezekana vipi Mmarekani akafanya jambo hili kwa kwa taifa lake mwenyewe?) mmoja wa wapelelezi wa FBI aliuliza kwa mshangao.
“Probably he was also one of the terror agents!” (Labda nae alikuwa mmoja wa mawakala wa magaidi)
*****
Jioni ya siku hiyo hiyo habari za kulipuliwa kwa jengo la WTC zilisambaa si Marekani tu bali dunia nzima, katika jiji la Washington watu wote walijua tayari David Syndrome alikuwa amekufa katika moto ule na televisheni za Marekani zilitangaza juu ya kikaratasi kilichokutwa katika gari lake lililokuwa limeegeshwa karibu na jengo la WTC lililolipuka.
Siku hiyo hiyo Rais George Bush alimtangaza gaidi Osama Bin Laden kuwa mtuhumiwa namba moja wa milipuko hiyo na siku chache baadaye alitangaza kutaifishwa kwa mali za magaidi na washirika wao waliwao ndani ya Marekani.
Kwa kikaratasi kilichokutwa ndani ya gari la David Syndrome serikali ya Marekani ilimtilia shaka kuwa alishiriki katika ulipuaji wa jengo hilo na kulazimika kukizuia kiwanda chake kufanya kazi nchini Marekani kama agizo la Rais lilivyokuwa wakati serikali ikiendelea na uchunguzi kama kweli alihusika au la!
****
Kwa hali walizokuwa nazo watu waliookolewa mara ya kwanza kutoka katika jengo hilo ilikuwa si rahisi kuamini kuwa walikuwa hai, sababu walikuwa ni nyama tu! Hivyo walipelekwa moja kwa moja chumba cha maiti.
Lakini saa sita usiku siku ya milipuko David Syndrome alishtuka na kujikuta amegandamizwa na vitu kama magunia mazito na alihisi kuwa katika baridi kali, alishindwa kuelewa alikuwa wapi mahali pale, kumbukumbu zilipomrejea nusu saa baadaye alikumbuka tukio zima lilivyotokea akasikitika kuona bado alikuwa akiishi.
“My God I’m still alive!”(Mungu wangu bado naishi!)
Aliyokuwa akiona kama magunia hayakuwa magunia bali maiti za watu zilizolazwa juu yake!
David Syndrome alipiga kelele kuomba msaada na wafanyakazi wa chumba cha maiti waliifungua friji alilokuwa amehifadhiwa na kumtoa mwili wake wote ulijaa damu na alikuwa na majeraha karibu kila sehemu ya mwili wake alijifananisha na maiti zilizofufuka katika filamu ya thriller iliyochezwa na Michael Jackson!
“Come out!”(Njoo nje) wafanyakazi wa chumba cha maiti hawakuamini kuwa palikuwa na mtu aliye hai katika jokofu lile.
“Are you alive?”(Wewe upo hai?)
“Yeah, but I want to die!(Ndiyo lakini nataka kufa!)
“Why?”(kwanini?)
“Because I killed a lot of people!”(Kwa sababu niliua watu wengi sana)
“How?”(Uliwauaje?)
“I know myself!”(Najua mwenyewe!)
Wafanyakazi wa chumba cha maiti walimchukua na kumpeleka moja kwa moja hadi wodi ya chumba cha wagonjwa mahututi ambako alipokelewa na kuanza kuhudumiwa na daktari.
“What is your name?”(Jina lako nani?)
“I’m David Syndrome?”(Mimi ni David Syndrome!)
“David Syndrome? David Syndrome the rich?”(Syndrome? Syndrome yule tajiri?)
“Yeah!”(Ndiyo)
“Is it?’(Kweli) daktari yule hakuamini kabisa kuwa mtu yule alikuwa ni David Syndrome sababu alishatangazwa tayari kuwa alikufa katika tukio hilo aliwangalia vizuri na kugundua kweli alikuwa ni yeye na kumpa pole.
Alibebwa harakaharaka na kupelekwa katika chumba cha upasuaji lakini njiani aliendelea kusisitiza kuwa yeye alitaka afe sababu aliua watu wengi sana, kauli hizo kutoka kwa mtu aliyeheshimiwa na kila mtu katika jiji la Washington zilimfanya daktari aamini kuwa iliwezekana David Syndrome alishiriki katika ukatili huo.
Serikali iliagiza David Syndrome atibiwe ipasavyo ili apone na kuwataja washirika wote wa ulipuaji ule na kweli baada ya siku kama ishirini na moja hivi David Syndrome alikuwa na hali nzuri ya kuongea na waandishi wa habari.
*****
Mamia ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliamini kuwa tajiri David Syndrome alishiriki katika mauaji hayo na walijaa katika ukumbi wa mikutano wa hospitali ya New York Medical Institute ambako David Syndrome alilazwa akiendelea kupata matibabu.
Waandishi walitaka kusikia ni akina nani hasa walishiriki katika kufanya ukatili huo sababu mpaka wakati huo serikali ya Marekani iliendelea kumtaja Osama Bin Laden kama mtuhumiwa namba moja ingawa haukuwepo ushahidi wa kutosha kama Osama alishiriki au la!
Masikio ya Marekani na ya watu wote duniani nzima yalikuwa nyuma ya redio na Televisheni zao kuangalia na kusikiliza kitu ambacho tajiri David Syndrome angekisema, kila mtu alitarajia lazima angetaja mtu aliyeshirikiana nae katika ulipuaji huo wa kigaidi na wengi walitaka kujua ni kwanini aliamua kuisaliti nchi yake.
Swali la kwanza katika mahojiano hayo lilitoka kwa mwandishi wa gazeti la New York Times aliyetaka kujua ni kwanini aliamua kuua watu wasio na hatia.
“I didn’t do anything as a terrorist!”(Sikufanya kitu chochote cha kigaidi).
“Then how did you kill?”(Sasa uliuaje?)
“It is me, Suzzane and professer Daniel Owo from Nigeria, we wanted to be rich, we wanted to win Bill Gates Economically! So we made the HTLV virus, which is killing the people around the globe, because of that sin I wanted to die, the disease we made is also killing me!”(Ni mimi, Suzzane na profesa Daniel Owo kutoka Nigeria, tulitaka kuwa matajiri kumshinda Bill Gates! Kwa hiyo tukatengeneza mdudu wa Ukimwi ambaye anaua watu hivi sasa, kwa sababu ya dhambi hiyo nilitamani kufa na ugonjwa nilioutengeneza ndio unaniua mimi) Waandishi wote wa habari walipigwa na butwaa kusikia jambo hilo.
Hakuna aliyetegemea kusikia jibu hilo kutoka kwa tajiri David Syndrome alikuwa amejaa makovu mwili mzima, dunia nzima ilishikwa na mshangao kugundua kuwa yeye ndiye mtu aliyekuwa akiwaua watu bila makosa!
Watu walishindwa kuelewa ni kwanini hasa aliamua kufanya unyama huo na kuteketeza viumbe wasio na hatia dunia nzima ililia machozi.
*****
Tajiri David mbele ya sheria:
Mahakama ilikuwa imejaa watu waliotaka kujua nini ingekuwa hatima ya mtu aliyeitesa dunia, tajiri David alikuwa akilia hakulia kwa sababu ya kuogopa adhabu iliyokuwa mbele yake bali aliendelea kuwaonea huruma binadamu waliokuwa wakiendelea kufa kwa makosa aliyoyafanya yeye.
Mawakili waliendelea kulumbana kisheria, upande wa utetezi ulionekana kushinda hivyo kuwa na uwezekano wa tajiri David kuachiwa huru.
Hakimu alipomgeukia David kumuuliza alikuwa ana lipi la kuiambia mahakama, pamoja na kuwepo dalili zote za ushindi kwa juhudi za mawakili wake alimwambia hakimu kuwa alistahili kufa.
Hakimu alitumia maneno yake kutoa hukumu, watu wote walikuwa kimya kusikiliza hukumu ambayo Jaji angetoa.
“Kwa kosa ulilolifanya unastahili kifo kwa kudungwa sindano ya sumu!” Jaji alimwambia tajiri David na watu wote walishangilia.
“Lakini mheshimiwa Jaji nisingependa kufa peke yangu,ni vyema Profesa Daniel Owo akasakwa pia kwa sababu dhambi tuliyofanya ni kubwa mno! Ni heri Suzzane yeye tayari ni mavumbi”
Je nini kitaendelea?
Tukutane Jumatatu mahali hapa
Unaweza kushaili ya marafiki zako.

No comments