Header Ads

KABLA SIJAFA LAZIMA DUNIA INISAMEHE- 4


“Sasa hebu niambie huo mkataba tunausaini lini?”
“Wakati wowote wewe ukiwa tayari ili mradi utuhakikishie kama kazi hiyo utaiweza!”
“Nimekwishawaeleza kuwa hilo kwangu mimi si tatizo hata kidogo, mimi ni Microbiologist bwana!” Alijigamba profesa Owo.
“Basi kesho njoo ofisini kwangu tumalize kusaini mkataba ili ulipwe pesa za kutanguliza ambazo ni paundi milioni moja sawa? Lakini naomba usimwambie mtu yoyote juu ya jambo hili kama unataka kuendelea kuishi?”
“Hamna matatizo!”
Siku hiyo profesa Owo alirejea nyumbani kwake akiwa na furaha kupita kiasi, mke wake alijaribu kumdadisi ni nini kilikuwa chanzo cha furaha ile lakini profesa hakuwa tayari kumueleza ukweli kila alipokumbuka kiapo alicholishwa na David Syndrome!
“Why are you so happy tonight?” (Kwa nini una furaha sana usiku wa leo?)
“Me?” (Mimi?)
“Yes you!” (Ndiyo! Wewe)
“Ah! It is because…..you know…..!” (Ah! Ni kwa sababu ya...unajua...!) Profesa alijaribu kumchenga mkewe kimaelezo ili tu asiutoboe ukweli wa furaha yake!
“Please hubby tell me why are you so happy (Tafadhali mpenzi wangu hebu niambie ni kwanini una furaha kiasi hicho?)
“I’m just happy as usual(Nina furaha kama ilivyokuwa kawaida yangu!)
“No! There must be something darling!”(Hapana lazima kuna kitu mpenzi)
“We are just going to be rich!”(sasa tutakuwa matajiri!)
“Rich?”(Matajiri?)
“Yeah!”(ndiyo)
“How?”(Kivipi?)
“I cant tell you now, I think I will never tell you this?” (Siwezi kukuambia sasa na ninafikiri kuwa sitakuambia kamwe)
*****
Usiku wa siku hiyo ulikuwa ni mrefu kwa profesa Owo, usiku mzima hakusinzia akifikiria siku iliyofuata ingekuwaje kama kweli angeutia saini mkataba huo wa pesa ambayo hakuwahi kuwaza kama katika maisha yake angeweza kuikamata! kila profesa alipojaribu kujiuliza ni kwanini hasa tayari David na Suzanne walitaka awatengenezee mdudu huyo bila kupata jibu! Alijua wazi kuwa alitakiwa kutengeneza mdudu hatari, lakini alikuwa tayari kufanya hivyo sababu ya shida alizokuwa nazo.
“I don’t care if they use the virus to kill human beings, that is not my business! All I care is my money,anyway I will have to ask them a little bit question!” (Mimi sijali hata kama watamtumia mdudu huyo kuua binadamu, hiyo tena mimi haitakuwa shughuli yangu ili mradi tu mimi nipewe pesa yangu, lakini nitajaribu kuwauliza maswali kidogo kukicha!)
Siku iliyofuata asubuhi ilikuwa tofauti na siku nyingine zote profesa alikuwa mtu wa kwanza kuamka kitandani na kuingia bafuni kuoga.
“This is unsual there must be something!”(Hii siyo kawaida ni lazima kuna kitu kinachoendelea)
Alipotoka bafuni kuoga profesa Owo alifikia kwenye maswali mazito kutokana na mkewe aliyetaka kujua ni nini hasa kiliendelea.
“I have told you there is nothing, why do you keep on asking questions’(Nimekwishakueleza hakuna kitu lakini kwanini unaendelea kuniuliza maswali?) Alijibu profesa Owo kwa ukali, kitu kilichomfanya mkewe aliyekuwa tayari mzee kuliko yeye anyamaze kimya!
Baada ya kuvaa profesa Owo alikaa mezani na kufungua kinywa, tayari kwa safari ya kwenda ofisini kwa David Syndrome alipoangalia saa yake ukutani aligundua ilikuwa bado saa mbili na nusu na yeye aliambiwa afike pale saa tatu na nusu.
“Sitaki kuwahi sana wasije wakaniona nina shida nyingi”Aliwaza profesa Owo.
Mawazo hayo yalimfanya profesa Owo arudi tena ndani na kuketi kitini lakini muda wote aliangalia saa ya ukutani, ilipotimia saa tatu kamili aliamua kuondoka na kutembea taratibu hadi ofisini kwa David na Suzanne, alifika pale ilikuwa tayari saa tatu na dakika kama thelathini na tano hivi, alisubiri mapokezi Suzanne na David waliwasili.
“Samahani tumechelewa kidogo sababu ilibidi tupitie benki kidogo vipi umekuja na mfuko mkubwa?”
“Wa nini?”
“Kubeba pesa zako!” Alisema David Syndrome huku akitabasamu!
“Jamani acheni utani mimi mwenzenu nipo siriasi, mnanielewa lakini?”
“Haya basi ingia huku ndani, profesa tumalize hii kazi!” Suzanne alimwambia profesa Owo nae akanyanyuka na kuwafuata ofisini walikoingia muda mfupi baadaye mwanasheria wa David na Suzanne aliingia ndani akiwa na makabrasha yake mkononi na kumsalimia profesa.
“Ready?”(Tayari?) David alimuuliza wakili wake.
“Yes sir(ndiyo mzee)
Wakili alitoa maelezo kidogo kwa profesa Owo juu ya mkataba huo, profesa alikaa kimya akiwa bado haamini kilichotaka kutokea.
“But why I you doing this? Don’t you know the virus will be dangerous to human beings including you?”(Lakini kwa nini mnatengeneza mdugu mbaya kama huyu, hamuoni kama anaweza kuwa hatari kwa maisha ya mwanadamu ikiwemo wewe?)
“Do you need the money professor?(Unahitaji pesa?)
“Yeah!”(ndiyo)
“Then don’t ask that Question anymore and never tell anybody about this job if you value your life on this planet(Basi usiulize tena swali hilo kama kweli unayathamini maisha yako)
“Ok!”(Sawa profesa Owo alikubali na baadaye alisaini mkataba huo kwa masharti ya kutengeneza mdudu huyo katika muda wa mwezi mmoja tu na baadaye alipokea pesa yake nusu ya aliyoahidiwa.
“At last I’m rich!”(Mwisho nimetajirika) Profesa aliruka juu na kujikuta akitamka maneno hayo.
“Ha!” Suzanne alimshangaa sana profesa kwa kitendo cha kushangilia pesa ile, kwake kilikuwa kiasi kidogo sana cha pesa.
“Zitakazobaki utalipwa lini?”
“Utakapomaliza kazi.”
Siku hiyo alipotoka ofisini kwao profesa alikwenda moja kwa moja benki ambako aliziingiza pesa zote na kubaki na paundi elfu moja aliyokwenda nayo nyumbani.
Siku hiyo mke wake alishangaa sana kumwona profesa akiwa na pesa nyingi kiasi kile na muda mfupi baada ya kufika wote wawili walitoka kwenda baa ya jirani ambako walinunua chupa kumi za waini na kurudi nyumbani.
“To lets celebrate my dear wife today is the day we say goodbye to poverty !”(Tusherehekee mke wangu leo ni siku tunauaga umasikini)
“What do you mean?”(Una maana gani kusema hivyo?)“I mean goodbye povert!” (Ninaamanisha kwaheri umasikini)
Mke wake alibaki mdomo wazi hakuelewa maneno aliyoyasema profesa! Siku hiyo walikunywa mpaka mchana wote na usiku kucha, walikesha wakinywa na kucheza muziki! Mke wake alizidi kushangaa kilichokuwa kimempata mume wake.
*****
Asubuhi siku iliyofuata profesa alianza usafi wa moja wa chumba chao ambako alianza taratibu kutengeneza maabara baada ya usafi alikwenda benki akachukua pesa na kununua vifaa vya kupimia wadudu mbalimbali katika maduka ya vifaa vya maabara!
Ilimgharimu karibu paundi elfu kumi kukamilisha maabara ya kisasa, ilikuwa ni pesa nyingi sana lakini hakuwa na la kufanya sababu alishaamua kufanya kazi hiyo tena kwa malipo makubwa!
Siku hiyo hiyo usiku profesa alikesha maabara akikuna kichwa chake katika kazi ya kutengeneza kirusi kilichotakiwa na matajiri David na Suzanne!
Aliotesha wadudu wengi sana na kuwakuza ndani ya kifaa kilichoitwa Incubator, kazi aliyoiita culture.
Siku saba baadaye usiku na mchana alikuwa akifanya kazi katika maabara yake na mkewe alikuwa bado akishangaa nini profesa alikuwa akifanya! Alikuwa tayari amekwishaotesha virusi vya aina mbalimbali na bakateria kama Staphylococci, Diprococci, Meningococci, Rubella virus, Measles virus na wadudu wengine wengi.
Hiyo ilikuwa hatua ya kwanza ya kazi yake na alipata matumaini ya kuikamilisha kazi hiyo kabla ya muda waliopangiana.
Siku ya nane alianza kuchanganya wadudu mbalimbali kumtengeneza mdudu aliyetakiwa lakini kila mdudu aliyemtengeza hakufanana, ndipo baadaye alipochanganya mdudu wa Nyani, kirusi cha surua na kirusi cha Kondoo ndipo alipompata mdudu mmoja mkali sana.
“Nafikiri huyu atawafaa!” Aliwaza profesa, hiyo ilikuwa ni siku kumi na tano tu baada ya kupewa kazi hiyo iliyotegemewa kufanyika kwa mwezi mzima, profesa alijisikia furaha ya ajabu!
Alikamata simu yake na kuwapigia David na Suzanne
“Tayari! Nawaomba mje hapa upesi na mje na pesa yangu kabisa!”
“Unasema kweli?”
Dakika chache tu baadaye walishafika na kushuhudia kazi aliyoifanya.
“Sasa tutajuaje kama atafaa?”
“Ni lazima tufanya majaribio!”
“Kwa nani?”
“Tafuteni mtu yoyote mmlete tumwigizie wadudu hawa muone watakavyomvuruga!”
“Tutamtoa wapi mtu atakayekubali?”
“Sielewi mtakapomtoa lakini ni lazima tufanye majaribio!”
“Tutatafuta mtu!”
*****
Siku iliyofuata David na Suzanne walijifanya wanamchukua kwenda nyumbani kumpa msaada ombaomba mmoja waliyekutana naye njiani, alikuwa ni mama wa makamo tena alikuwa kipofu.
“Ingia kwenye gari tukakupe msaada nyumbani!” Bila ubishi mama yule alipanda, baada tu ya kuingia garini walimpulizia dawa ya usingizi akalala na kumpeleka moja kwa moja nyumba kwa profesa Owo ambako alidungwa sindano iliyojaa wadudu aliowatengeneza kwenye mshipa wa damu.
“Tayari! Nyie mrudisheni mtaani halafu muwe mnamuangalia maendeleo yake! atakonda kama spoku!”
David na Suzanne walimbeba ombaomba yule akiwa usingizini na kuondoka naye hadi hospitali ambako walijifanya wasamaria wema waliomuokota mtaani.
*****
Walipozaliwa mapacha Dorothy na Johnson kila mtu alikiri Alfred na mkewe Elizabeth walizaa watoto wazuri sana, kila mtu alipenda kuwabeba watoto hao, walikuwa ni mapacha waliofanana mno ingawa mmoja alikuwa wa kiume na mwingine wa kike! Na walipovalishwa nguo za kike ilikuwa si rahisi kugundua kuwa Johnson alikuwa mtoto wa kiume, watoto wote walikuwa wazuri kupita kiasi!
“Watoto wenu wazuri mno hivi wa kiume ni yupi?”
“Huyo uliyembeba wewe!”
“Huyu ni wa kiume jamani? Liz umezaa watoto wazuri sana!” Rafiki mkubwa wa Liz, Agripina alimwita Elizabeth kwa kifupi akiwasifia watoto wake!
“Huyu wa kiume akikua ndiye atakuwa Mr University na huyu wa kike ndiye atakuwa Miss Uganda!”
‘Hongera sana hivi sasa wana kilo ngapi ?’
‘Wote wawili wana uzito sawa wa kilo kumi na tatu kila mmoja’
‘Umri wao?”
“Mwaka mmoja!’
“Aisee!”
****
Ni kweli Johnson na Dorothy walikuwa mapacha wa kuvutia, katika umri wa miaka mitatu tu tayari walishaanza kuwa watoto nyota nchini Uganda, sura zao zikitumika katika matangazo ya maziwa ya Cowboy!
‘Watoto wazuri ? Watoto wazuri! watoto wazuri!” Hiyo ndiyo ilikuwa kauli iliyosikika midomoni mwa karibu kila mtu aliyeliona tangazo la maziwa ya Cowboy, wazazi wengi walitamani kuwa na watoto kama wao.
Kila mtu alipenda sana kuwabeba watoto wale na hata katika shule ya chekechea waliyosoma walimu waliwapenda sana watoto hao!
‘They are like Black Americans! (Ni kama Wamarekani weusi!) Ndivyo walimu walivyosema kila siku, walikuwa ni watoto ambao ilikuwa si rahisi kuwazoea.
****
“Mpenzi sihitaji watoto zaidi, Johnson na Dorothy wananitosha” Alisema Alfred
“Hapana mume wangu, tunahitaji kupata watoto wengine wawili zaidi, hujui kitakachotokea Kesho, tafadhali tuzae wengine wawili zaidi,” Elizabeth alisisitiza.
“Hebu angalia mke wangu, Bill Clinton ni gavana wa huko Marekani ana mtoto mmoja kwa nini sisi tuwe na watoto zaidi ya wawili?” Aliuliza tena Alfred.
Watoto wao walikuwa wametimiza umri wa miaka sita na Elizabeth alitaka wadogo zao lakini mumewe alikataa kata kata na mwisho wa maongezi yao walikubaliana kufunga kizazi tena wote wawili.
Siku iliyofuata wote walikwenda kwenye cliniki ya uzazi wa mpango kutimiza azma hiyo!
‘We need no more children so we have come to tubal ligation and vasectomy! (Hatuhitaji watoto zaidi kwa hiyo tunakuja kufunga uzazi sisi sote wawili)
‘Sure” (Hakika)
“Then you are an example in Uganda (Kama ni hivyo basi nyinyi ni mfano Uganda hii)
Baada ya maongezi hayo wote wawili walipelekwa chumba kidogo cha upasuaji ambako walifanyiwa upasuaji wa kuziba mirija yao ya mayai na walipoondoka hospitali siku mbili zilizofuata wote wawili hawakuwa na uwezo wa kuzaa tena!
Sasa ni wajibu wetu kutumia kila kitu tulichonacho kuwalea watoto wetu, ni lazima wapate elimu sawa na ninataka wasome hadi chuo kikuu na siyo hapa Uganda bali Marekani au Uingereza kama mimi nipo hai ni lazima ndoto hii itimie!”
*****
Ombaomba alipozinduka baadae alijikuta bado yupo mtaani, alishindwa kuelewa ni nini kilichompata mpaka akafikia hali ile, lakini baadae kumbukumbu zilipomrudia alikumbuka kubebwa katika gari lakini hakukumbuka ni gari la nani lililombeba na alishindwa kukumbuka alirudi vipi hadi mtaani.
Ombaomba yule hakujali ili mradi alikuwa mzima na asubuhi kulipokucha aliendelea na kazi yake ya kuomba barabarani kama ilivyokuwa kawaida yake na hakugundua tofauti yoyote iliyokuwa imetokea mwilini mwake.
Kwa wiki nzima aliendelea kuwa mzima wa afya, profesa Owo, David Sydrome na Suzana wakiendelea kuifuatilia afya yake kila walipopita mtaa ule ilikuona ni nini kingempata ombaomba yule baada ya kumchoma sindano ile yenye virusi vilivyotengenezwa na Profesa Owo.
Wiki ya pili ombaomba yule alianza kugundua tofauti fulani ikitokea mwili mwake! Kitu cha kwanza kilichojitokeza kilikuwa ni uchovu wa mwili wake, baadae alianza kuharisha na pia kukohoa.
Wiki ya tatu omba omba yule alianza kupungua uzito kwa kasi na alianza kupatwa na majipu pamoja na homa kali za kila jioni, afya yake iliharibika na kujikuta akishindwa kufanya kazi yake ya kuomba.
Wiki nne ilipofika alikuwa amekondeana kupita kiasi, alikuwa hawezi hata kunyanyuka, akawa anashinda amelala pembeni mwa barabara baadaye alichukuliwa na wasamaria wema na kupelekwa hospitalini ambako aligundulika kuwa na kichomi au Pnemonia! alianzishiwa matibabu lakini hayakusaidia kwani siku ya tano tu alifariki dunia akiwa amebaki mifupa tupu.
Kifo chake kilikuwa furaha kubwa sana kwa Profesa Owo, David Sydrome na Suzane walihisi ushindi mkubwa mioyoni mwao! Tayari waliuona utajiri ukiwa mlangoni mwao, kwa mpango waliokuwa nayo kichwani miaka kumi au kumi na tano baadaye wangekuwa matajiri kuliko Bill Gate hivyo wangeirudisha sifa yao kwa mara nyingine.
“Hongera Profesor kazi yako ni nzuri lakini bado kuna kitu kimoja tu unatakiwa ufanye!”
“Kitu gani hicho?”
“Wapunguze nguvu kidogo hao virusi ili wawe wanachelewa kidogo kuwauguza na pia washambulie taratibu ili wagonjwa wachelewe kidogo kufa! huyu kafa haraka mno tofauti na mategemeo yetu!”
“Sasa mnataka mtu awe anaugua baada ya muda gani na afe baada ya kipindi gani?’
Baada ya miaka mitano hadi kumi na tano! Na aendelee kuteseka kwa muda usiyopungua miaka mitano!
“Hiyo ni kazi ndogo sana kwangu hebu nipe siku tatu”
Waliachana na Profesor akiingia maabara alipotoka huko baada ya siku hizo tatu kazi alishaimaliza na kukabidhiwa pesa yake iliyokuwa imebaki.
“Hakuna siri ya watu wawili duniani, hili jambo ni lazima siku moja litavuja tu, siwezi kukaa tena hapa Uingereza narudi kwetu Nigeria, watu wakifa sana kwa virusi nilivyotengeneza ni lazima siri hii itagundulika halafu nitakuwa matatizoni! Nikifika Nigeria nitabadilisha jina na hakuna mtu atakayegundua kuwa mimi ndiye Profesor Owo!”Aliwaza profesa Owo.
Mwezi mmoja baadae Profesor aliondoka Uingereza bila kumuaga mtu yoyote na watu hawakujua alikwenda wapi! Alirudi kwao Nigeria ambako alianzisha shirika lake la utafiti wa magonjwa na baadae kufungua hospitali binafsi zilizompatia pesa nyingi na kufanya awe tajiri, hakuna mtu yeyote aliyejua siri ya utajiri wake, watu wote walimwogopa na kumheshimu.
****
“How will we get the virus into the people’s bloods!”(Tutawafikishaje wadudu hawa katika damu za watu?)
“Ni rahisi sana nitazungumza na daktari Cornel McLain kama ataturuhusu tuwaingize wadudu kwenye chupa za chanjo ya kupooza ambayo itatolewa kwa watoto watakaugua ugonjwa huu baadaye maishani mwao” Alijibu David Syndrome.
“Hilo ni wazo zuri sana” aliongeza Suzanne na wote walimpigia simu Dr. McLain ambaye alikubali kufanya jambo hilo kwa malipo ya dola milioni tano.
“But please make sure the Vaccine is not given to the kids in the Uk!”(Lakini hakikisheni chanjo hiyo haitolewi kwa watoto hapa Uingereza)
“The vaccine will be shipped into Africa where the African kids will be given the vaccines! Who cares about the Africans let them die, and they are the once to buy our drug when they start suffering”(Chanjo hii itapelekwa Afrika ambako watoto watachanjwa! Kwanini nani anawajali Waafrika wakifa? Ni wao watakaonunua dawa zetu wakianza kuugua)
“For how long will the virus will stay in their blood before they become sick?” ( Virus hivi vitakaa mwili mwao kwa muda gani kabla hawajaanza kuugua?)
“Approximately 5 – 10 years!” (Mkadirio ya miaka mitano hadi kumi)
“Oh! that’s a long incubation period. (Oh! Huo ni muda mrefu sana)
“But how are we gonna do this in Africa?” (Lakini tutalifanyaje zoezi hili Africa?”
‘We shall convice African Leaders to start a Campaign against Polio to all the kids under ten years” (Tutawashawishi viongozi wa Afrika waanzishe kampeni dhidi ya kupooza na watoto wote chini ya miaka kumi watachanjwa)
Wakati daktari McLain akipokea pesa alizopewa machozi yalikuwa yalimtoka, aliwahurumia sana watoto wa Afrika, lakini hakuwa na lakufanya,pesa aliitaka sana!
“What is the name of the virus?” (Jina la kirusi hiki ni lipi?)
‘We dont know yet, Professor Owo didn’t tell us!” (Hata sisi hatujui Profesa Owo hakutueleza)
Miezi miwili baadae chanjo ya kupooza iliyokuwa na virusi hivyo ilikuwa nchini Uganda! Na kampeni likuwa ikiendelea. Katika muda wa mwezi mmoja tu watoto karibu 300,000 chini ya umri wa miaka kumi walikuwa wamechanjwa dawa hiyo yenye virus hatari bila wazazi wao kujua! Laiti wazazi wao wangefahamu wasingediriki kuwapeleka watoto wao waliowapenda kuchanjwa dawa, hivyo ilikuwa ni sawa na kuwanyonga watoto wao.
*****
Kesho ni lazima tuwapeleke Johnson na Dorothy wakachanjwe chanjo ya polio! Siku zote hizi tumekaa hapa hatuwapeleki wakati watoto wengine wanachanjwa dhidi ya ugonjwa huo wa kupooza, tutafanya nini wakati watoto wetu wakiugua polio wakati watoto wenyewe ni hawa tu?’
‘Kweli mume wangu huu ni uzembe mkubwa sana ni lazima kesho niwapeleke si chanjo zinatolewa hata siku ya Jumapili ?’
‘Ndiyo !’
‘Basi kesho !’
Yalikuwa ni maongezi kati ya Elizabeth na Alfred wakiongelea kuwapeleka watoto wao pekee kupata chanjo hiyo hatari kwa maisha ya watoto wao, kwa walivyowapenda watoto wao siku zote hawakutaka wapatwe na tatizo lakini tayari walikuwa wakiwapeleka watoto wao kuwachanja na mdudu hatari aliyemuua ombaomba! Hawawezi kuwapata watoto wengine tena?
Je, kitatokea?
Je Mapacha Johnson na Dorothy watachanjwa? Je watakufa? Fuatilia Ijumaa

No comments