Header Ads

KABLA SIJAFA, NAOMBA DUNIA INISAMEHE-5


Redio zilitangaza na magazeti yaliandika kuhamasisha juu ya chanjo hiyo ya polio nchini Uganda, Wazazi wengi waliowapenda watoto wao walijitokeza na kufurika katika vituo mbalimbali kwa chanjo kuwachanja watoto wao dhidi ya ugonjwa huo hatari.
Wauguzi na madaktari nao walifanya kazi kwa bidii kuwachanja raia wa Uganda bila kujua walikuwa wakiwaua watu wao wenyewe! Walikuwa wakiua nguvu kazi yao Uganda siku za usoni.
“Hallaa Hallaa! David Syndrome alichekelea kila alipopokea ripoti kuwa idadi kubwa ya watoto walichanjwa kila siku nchini Uganda na chanjo hiyo iliyokuwa na wadudu hatari.
Jumapili asubuhi
Elizabeth na mumewe Alfred walikuwa miongoni mwa watu walifurika katika kituo cha chanjo cha Ibisigera kilichopo nje kidogo ya mji wa Kampala, iliwalazimu kwenda kwenye kituo cha nje sababu siku hiyo ya jumapili watu wengi sana walipeleka watoto wao kuchanjwa na kufanya vituo vingi vya mjini kufurika na kufanya upatikanaji wa chanjo kuwa ngumu sana!
“Afadhali huku watu ni wachache kidogo!” Alfred alimwambia mkewe Liz wakati wanaingia kituoni.
Akinamama wengi walikuwepo kituoni, watoto walisikika wakilia ndani ya jengo la kituo, inawezekana walilia sababu walijua walikuwa wakiingiziwa vifo mwili mwao, wakati wanalia hivyo mama zao bila kujua walifurahia kitendo hicho walichoamini kilikuwa cha kuwakinga watoto wao na kuwaongezea maisha.
Liz na Alfred walijipanga kwenye mstari, wote wakiwa wamewabeba watoto wao mikononi wakisubiri zamu yao kuingia kwenye chumba cha chanjo!
“Haya ingieni ndani nyie si mpo pamoja?” Muuguzi aliwauliza Alfred na mkewe nao walinyanyuka na kuanza kuingia ndani.
“Watoto wenu ni wazuri sana!”
“Asante!”
“Tena naona ni mapacha au sivyo?”
“Ndiyo ni mapacha!”
Si Alfred wala Elizabeth aliyejua wala kuhisi kuwa walikuwa wakiwapeleka watoto wao kwenye kifo! Walijua waliwapeleka watoto wao kuwakinga! Walipoingia ndani walikaa chini na manesi walianza kazi ya kuwachanja watoto wao chanjo ilipoingia tu miilini mwa Dorothy na Johnson walianza kulia kwa sauti ya juu.
“Mbona watoto wanalia kiasi hiki?” Liz alimuuliza muuguzi aliyewachanja Doroth na Johnson.
“Hata sisi tunashangaa ni kwanini chanjo ya polio ya safari hii inawaliza watoto kiasi hiki, siyo kawaida ya chanjo hii!” Hata muuguzi alionyesha wazi kuwa na mshangao.
Wiki moja kufuatia chanjo hiyo hospitali zote nchini Uganda zilifurika watoto wengi, watoto wote waliochanjwa chanjo ya polio walikuwa wagonjwa wa homa kali kupita kiasi! Madaktari na wizara ya afya walishangazwa sana na hali hiyo kwani ilikuwa si kawaida wa chanjo ya polio kusababisha matatizo kiasi kile!
Hakuna hata mtoto mmoja aliyepoteza maisha kutokana na chanjo hiyo homa zote zilikwisha na watoto waliendelea vizuri.
*****
“Hallow Suzanne!”
“Ndiyo Suzanne sema”
“Shughuli ilikwenda vizuri, labda watoto lakini tatu walichanjwa na chanjo Uganda.”
“Kweli?”
“Ndiyo na hii ina maana miaka kumi na tano kuanzia hivi sasa tutakuwa matajiri wakubwa, Bill Gate atakuwa chini yetu!”
“Baada ya kampeni hii ya chanjo tutafanya nini sasa?”
“Tutaanzisha kampuni ya madawa itayokuwa ikifanya utafiti wa dawa ya kuongeza urefu wa maisha ya watu watakaoathirika na mdudu huyo”
Mwezi mmoja baada ya maongezi hayo katika simu David na Suzanne walianzisha kampuni ya utafiti wa madawa ya binadamu na wakaajiri wataalam ambao baada ya kuonyeshwa mdudu aliyetengenezwa na profesa Owo katika darubini walianza kazi ya kuitafuta dawa hiyo kwa miaka mitano mfululizo walikuwa bado hawajafanikiwa kupata dawa ya kumpunguza nguvu mdudu huyo ili kuongeza maisha ya mgonjwa!
David na Suzanne walitamani profesa Owo angekuwepo lakini hakupatikana mahali popote, walihisi angekuwa Nigeria lakini ilikuwa si rahisi kumpata.
Mwaka mmoja baadaye walifanikiwa kugundua dawa hiyo waliyoiita ZAT, waliitunza dawa hiyo ndani bila mtu kufahamu! Ilibaki kuwa siri wakisubiri watu waathirike.
****
Miaka kumi baada ya chanjo ugonjwa wa ajabu uliibuka nchini Uganda na dunia nzima ilichanganyikiwa, wataalam walishindwa kuelewa ni ugonjwa gani uliokuwa umeingia duniani na shirika la Afya duniani lilipotuma wataalam wake nchini Uganda kufanya utafiti ndipo walipomgundua mdudu wa ajabu katika damu za wagonjwa na waliochunguza alikuwa ni mdudu gani waligundua aina ya virusi aliyeshambulia sana chembechembe nyeupe za damu aina ya T Lymphocytes na kufanya mgonjwa kukosa kinga na kuugua magonjwa yote!
Waliamwita mdudu huyo HTLV yaani Human T Lymphacites virus! Au Human Immunodeficiency virus na ugonjwa wa upungufu wa kinga uliosababisha waliuita AIDS au Acquired Immnodeficiency syndrome!
Vijana wengi nchini Uganda waliteketea na ilipogundulika kuwa ulisambazwa kwa kujamiiana vijana wengi waliliogopa sana tendo hilo!
Wanasayansi pamoja na kugundua mdudu huyo walishindwa kuelewa chanzo chake, walipoangalia katika orodha ya virus hapakuwahi kuwa na kirusi cha aina hiyo duniani, waliamua kumpitisha kama mdudu mpya katika uso wa dunia.
****
Wakati binadamu wakiendelea kufa Uganda, David Syndrome na Suzanne Leon walichekelea na kuona utajiri wao umefika! Wakati wao wa kupata pesa umefika! Lakini hali ilikuwa tofauti kwa profesa Owo ambaye wakati ho alijulikana kama chifu Onuku nchini Nigeria.
Alipoisikia taarifa juu ya vifo vilivyotokea nchini Uganda machozi yalimtoka, alijisikia mkosaji moyoni mwake, kwa kuua idadi kubwa ya watu kwa tamaa ya pesa! Alitamani hata kujitoa roho yeye mwenyewe, aliihurumia dunia kwa mdudu aliyemtengeneza dunia ingepatwa na pigo kubwa sana!
David Syndrome na Suzanne waliposikia habari ya vifo nchini Uganda walikuwa ni watu wa kwanza kuitangazia dunia kwamba walikuwa na dawa ya kuwaongezea maisha ya watu walioathiriwa na mdudu huyo hatari!
Jamii yote nchini Uganda ilizipokea taarifa hizo kama baraka kwa matumaini ya kupata dawa ya kutibu ugonjwa huo hayakuwepo kabisa, wataalam kila siku walikuna vichwa vyao kutafuta dawa ya kumuua mdudu huyo aliyeaminika kutokana na nyani yalizidi kupungua.
Kampuni ya madawa ya Suzanne na David ilitengeneza madawa mengi kwa ajili ya majaribio nchini Uganda na madawa hayo yalipotumiwa na wagonjwa yalionyesha matumaini makubwa na wengi walianza kuyatumia.
Mwanzoni yaligawiwa bure lakini baadaye yaliuzwa kwa pesa, mgonjwa mmoja ili akukamilisha dozi alihitaji kiasi cha shilingi milioni mbili za Uganda! Watu walilazimika kuuza nyumba zao, magari yao, mashamba yao ili kupata dawa hiyo.
Kiwanda cha David Syndrome na Suzanne kilifanya kazi usiku na mchana kutengeneza dawa ya ZAT na Makontena karibu mia yalisafirishwa kuja Uganda na Afrika kila wiki! Ugonjwa wa Ukimwi ulizidi kusambaa Afrika na sasa ulikuwa ukiingia Tanzania sehemu za Bukoba na kwenye sehemu za Kyaka ambako wafanyabiashara wengi kutoka Uganda walikwenda kufanya biashara zao kwenye magulio.
Biashara ya madawa iliwaingizia David na Suzanne pesa nyingi sana, utajiri huo ulianza kuitisha tena duniani, kiasi kikubwa cha pesa kiliingia katika akaunti zao huko Uingereza utajiri wao ulianza kumtisha hata Bill Gate ikalazimu nae aingie tena chumba cha utafiti ili kugundua kitu kingine katika mfumo mzima wa kompyuta.
Bill Gate alijua mwaka 2000! Kompyuta zote zingezima kwa sababu ya kitu kilichoitwa Y2K! Aliingia chumba cha utafiti ili kutengeneza kifaa ambacho kingeziwezesha kompyuta kuendelea kufanya kazi bila kuzima hata baada ya mwaka 2000! Alijua kazi hiyo ingemwingizia pesa zaidi na kumfanya tajiri zaidi ya David na Suzanne!
****
David na Suzanne walikuwa waangalifu sana na maisha yao walijua tendo lolote la ndoa lingemsababishia vifo kutokana na mdudu waliyemtegeneza hivyo waliamua kubadili utaratibu wa kufanya mapenzi na kuanza maisha ya kishoga.
David akaanzisha uhusiano wa kishoga na wanaume wenzake, aliwachukua wanaume kumliwaza, sababu aliwaogopa wanawake Ukimwi na Suzanne naye ilikuwa hivyo hivyo hakutaka uhusiano na wanaume nae pia alianza uhusiano wa kisagaji na wanawake wenzake!
*****
David Syndrome alikuwa ndani ya gari lake akipita katikati ya jiji la London, kama ilivyokuwa kawaida yake alitamani wanaume wenzake na kufanya nao mapenzi, mara ghafla alimwona mvulana mmoja akipita pembeni ya barabara alikuwa na sura nzuri kupita kiasi, alilazimika kusimamisha gari lake na kumwita kijana yule.
“I’m David Syndrome what is your good name sir?” (Naitwa David Syndrome, unaitwa nani mkuu?)
“My name is Johnson Alfred!” (Naitwa Johnson Alfred)
“Where are you from?” (Umetoka wapi?)
“I’m from Uganda!” (Uganda)
“What are you doing here in London?”(Unafanya nini hapa London?)
“I’m studying at the University of West London!” (Ninasoma katika Chuo cha West London)
“Please get into my car!”(Tafadhali ingia garini twende)
“Where to?”(twende wapi?)
“I need to talk to you privately, do you know me?I’m the richest person in the United Kingdom, do you mind having dinner with me?”(Nahitaji kuongea na wewe faragha, mimi ni tajiri kuliko wote hapa Uingereza unaonaje ukila na mimi chakula cha usiku?)
“It is ok!”(Sawa tu)
Johnson alipanda ndani ya gari la David na safari ilianza mbele kidogo David alianza kumshika Jonathan sehemu za siri! Jambo lililomshangaza sana kijana yule.
“What are you doing?”(Unafanya nini sasa?)
“Ninakupenda na ninataka uwe mpenzi wangu”
“Don’t you know I’m your fellow man?”(Hujui kama mimi ni mwanaume mwenzako?)
“Even though!”(Pamoja na hayo!)
*****
Kwa utajiri mkubwa aliokuwa nao Suzanne Leon alifanywa ndiye mlezi na mfadhili mkuu wa chuo kikuu cha Newtown nchini Uingereza ni chuo hicho ndicho yeye pia alisoma, kila mara alitoa misaada mbalimbali kwa chuo hicho, ilikuwa ni misaada ya kifedha na ushauri wa miradi mbalimbali ya chuo hicho.
Suzanne aliheshimika kama mwanamke mwenye pesa kuliko wanawake wote nchini Uingereza, ilidaiwa alimzidi hata Malkia kwa utajiri ambao ulikadiriwa kuwa kiasi cha paundi bilioni nne na utajiri huo ulitokana na mauzo ya dawa ya ZAT, dawa ya kuongeza maisha kwa wagonjwa wa ukimwi, ambayo kiwanda chao na David Syndrome kilitengeneza.
Kila mtu nchini Uingereza alishangazwa na uvumbuzi wa Suzanne Leon na David Syndrome na walishangaa pia jinsi watu hawa walivyowahi kuivumbua dawa hiyo na kujipatia mamilioni ya paundi kirahisi na kuwa matajiri tena pamoja na kuwa walielekea kufilisika kabisa.
Watu wengi walijaribu kutengeneza dawa kama hiyo lakini walishindwa na hakuna aliyeweza kuiiga dawa hiyo, ingawa wengi walitamani kufanya hivyo ili kujipatia pesa zaidi, fomula ya kutengeneza dawa hiyo iliendelea kubaki siri ya David na Suzanne peke yao.
Pamoja na utajiri wote waliokuwa nao Suzanne aliwashangaza watu nchini Uingereza na wengi walishindwa kuelewa ni nini hasa maana ya pesa aliyokuwa nayo mwanamke huyo kwani hakuna aina yoyote ya starehe aliyoifanya, hakuwa na uhusiano na mwanaume yoyote yule na wala hakutaka kuolewa.
Wanaume wengi walimfuata kumtaka mapenzi lakini siku zote jibu lake lilikuwa ‘hapana’ hakuna mwanaume aliyefanikiwa kulipata penzi la Suzanne! Kwa miaka karibu sita Suzanne hakuwahi kukutana na mwanaume kimapenzi, siku zote alijiliwaza na msichana mmoja mwafrika aliyeitwa Dorothy Mwafrika kutoka Uganda aliyekuwa nchini Uingereza kusoma katika chuo kikuu cha Newtown ambako alikuwa akichukuwa digrii ya uchumi.
Yeye na kaka yake aliyeitwa Johnson walipelekewa na wazazi wao nchini Uingereza kusoma baada tu ya kumaliza elimu ya sekondari nchini humo ambako wazazi wao waliamini elimu ya chuo kikuu haikuwa bora!
*****
Kwa mara ya kwanza Suzanne alimwona Dorothy katika sherehe za mahafali ya chuo kikuu Newtown hicho alikokuwa amealikwa kutoa shahada na vyeti kwa wanafunzi waliokuwa wakimaliza katika chuo hicho na kupata digrii zao.
Siku hiyo Dorothy alipangiwa kusoma risala kwa mgeni wa heshima, aliisoma risala hiyo vizuri sana jambo lililomvutia sana Suzanne ambaye alilazimika kuomba muda wa kuongea na Dorothy baada ya sherehe hiyo na ndivyo ilivyotokea, Suzanne na Dorothy waliongea mengi sana na Suzanne aliezea jinsi alivyovutiwa na Dorothy pia alimsifia uzuri wake na ulaini wa ngozi yake.
Ni wakati huo ndio Suzanne aliyekuwa amesikia habari juu ya tabia ya wanawake kwa wanawake kuridhishana kimapenzi alitamani sana kufanya hivyo na Dorothy ili kujiepusha na mdudu hatari ambaye yeye na David pamoja na profesa Owo walimtegeneza!
Alikuwa na uhakika kabisa kuwa siku moja lazima mdudu huyo angereja Uingereza baada ya mzunguko wa muda mrefu isingewezekana abaki afrika peke yake.
Hiyo ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya Suzanne kutotaka kabisa kujihusisha na mambo ya kujamiiana na wanaume pamoja na kuwa alikuwa na utajiri wa kutisha.
Baada ya kumwona Dorothy na kuvutiwa nae akijua ni mwanafunzi kutoka Afrika ya Kusini mwenye shida nyingi, Suzanne aliamua kumwingiza katika mitego yake ili hatimaye amwingize katika mchezo mbaya wa Lesbianiasm au usagaji kama wengi walivyouita.
“One day you have to visit my home, when are you free?(Siku moja ni lazima utembelee nyumbani kwangu, lini una nafasi?)
“Me?”(Mimi?)
“Yes!”(Ndiyo)
“Probably next week, Sunday(Labda wiki ijayo jumapili sawa?)
“Ok! I will send my driver to pick you up!(Sawa nitamtuma dereva wangu kukuchukua)
“I will be anxiously waiting!”(Nitakusubiri kwa hamu kubwa sana!)Alijibu Dorothy.
Wakati wa kuondoka chuoni hapo Bi. Suzanne alimwachia Dorothy kadi yake ya biashara pamoja na paundi za kiingereza 5000! Zilikuwa ni pesa nyingi sana kwa Dorothy na alishangazwa sana na wema wa mwanamke huyo.
“In case of any problem call me, right?(Ukiwa na tatizo lolote tafadhali nipigie simu sawa?)
“No doubt, I will do it Miss Suzanne, Thank you for your kindness and God bless you(Bila shaka nitafanya hivyo, asante sana kwa ukaribu wako na Mungu akubariki)
Siku hiyo waliachana kwa amani na Dorothy hakustukia kitu chochote kuhusu nia ya Suzanne kwake na siku tatu baada ya kuondoka alipokea maua mazuri pamoja na kadi kutoka kwa Suzanne na alipofungua kadi hiyo alishangaa kukuta imeandikwa maneno ‘I love you’ kwa kiasi fulani alishindwa kabisa kuyaelewa maneno hayo lakini aliamua kuyachukulia kama maneno ya kawaida ambayo mama anaweza kumwambia mtoto wake!
Siku hiyohiyo jioni alipokea zawadi ya pete nzuri ya almasi na rubi ambayo pia ilizidi kumshangaza Dorothy.
Mambo mbalimbali yalizidi kutokea kabla siku ya kuonana haijafika na yalimtia wasiwasi mkubwa sana Dorothy lakini alishindwa kumwambia mtu yoyote na kukaa nayo moyoni mwake
*****
Siku ya ijumaa jioni ilijaa mawingu na kulikuwa na kila aina ya dalili kuwa mvua kubwa ingenyesha, baridi ilitanda kila sehemu na karibu kila mwanafunzi katika chuo kikuu cha Newtown alivaa sweta nzito!
Dorothy alikuwa kwenye simu akiongea na mtu kwa muda mrefu na alionekana kutabasamu na kuchekelea.
“Yes I’m waiting for that day!”(Ndiyo naisubiri siku hiyo tu!)
“I have prepared a lot of things for you and please understand that day you wont go back to the university as you and I will attending a party at my friends place!”( Nimekutayarishia mambo mengi sana na kumbuka siku ukija hutaweza kurudi tena chuoni kwa sababu mimi na wewe tutakwenda kwenye sherehe nyumbani kwa rafiki yangu)
‘No problem madame!”(Hakuna tatizo mama)
Mateso aliyokuwa ameyapata Suzanne kwa muda wa miaka mingi ya kukaa bila mpenzi yalikuwa yametoka na sasa alikuwa amekamia kuyamaliza kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwenzake na alikuwa amepania kumpata Dorothy kwa gharama yoyote na siku ya jumapili aliiona ilikuwa mbali sana.
“Siku hiyo akija tu ni lazima itokee!” Aliwaza Suzanne.
*****
Siku ya jumapili jioni kama walivyokuwa wamepanga Suzanne alimtuma dereva wake chuo kikuu cha Newtown kumfuata Dorothy na haikuchukua muda mrefu sana dereva akawa amerejea nyumbani kwa Suzanne akiwa na Dorothy aliyevaa sketi fupi iliyoyaonyesha mapaja yake nje na kufanya awe wa kusisimua zaidi.
“You’re welcome and feel at home!”(Karibu sana na ujisikie upo nyumbani)
“Thanks madamme!”(Asante sana mama!)
Dorothy alimheshimu sana Suzanne kwa sababu umri wake ulikuwa ni sawa na wa mama yake au alimzidi hata mama yake kwa umri kidogo! Hakuamini kujikuta katika nyumba nzuri kiasi kile, nyumba ya bi Suzanne ilipambwa na kila aina ya mapambo na mengine Dorothy hakuwa kuyaona katika maisha yake yote.
“Are you married Miss Suzanne? Suzanne umeolewa?)
“No, I’m not!”(Hapana)
“What happened?(Kilitokea nini?)
“Nothing I just decided to live alone!”(Hakuna kitu niliamua tu kuishi peke yangu)
“Are you not lonely?”(Je hujisikii ukiwa?)
“That’s why I need friends like you to make me feel happy!”(Ndiyo maana nahitaji marafiki kama wewe)
“I will make you happy because we’re friends(Kwa sababu sisi ni rafiki yangu nitakufanya uwe na furaha)
“Thank you my daughter and I promise to make your stay in the Uk happy too!”(Asante sana binti yangu na mimi ninaahidi kuyafanya maisha yako hapa Uingereza yenye furaha kubwa)
Baada ya maongezi ya muda mrefu nyumbani kwa Suzanne waliondoka kwenda kwenye sherehe iliyokuwepo nyumbani kwa mmoja wa marafiki wa Suzanne usiku huo, ilikuwa ni sherehe ya kifahari na Dorothy alijisikia vizuri sana kuwa mahali pale na alipata nafasi ya kusalimiana na matajiri wakubwa wa Uingereza na alitambulishwa kwa watu wengi sana katika sherehe ile na baadaye vyakula na vinywaji viliendelea kutumika.
Kitu pekee kilichomshangaza Dorothy katika sherehe ile ni kuwaona wanawake kwa wanawake na wanaume kwa wanaume wakiwa pamoja kama watu na wapenzi wao! Hapakuwa na mtu hata mmoja aliyekuwa pale na mtu wa jinsi tofauti.
Majira ya saa saba hivi za usiku watu wote ndani ya ukumbi huo walionekana kulewa chakali isipokuwa yeye peke yake, hata Miss Suzanne pia alikuwa hoi kwa pombe, watu wote ndani ya ukumbi huo walianza kuvua nguo na kubaki kama walivyozaliwa! Hata miss Suzanne naye alifanya hivyo na kubaki uchi mbele ya Dorothy.
“Miss Suzanne what are we doing here?”(Miss Suzanne tunafanya nini hapa?)
“This is a crazy lesbianis and homesexual party my daughter! you’re supposed to undress too!’(Hii ni sherehe ya mashoga na wasagaji mwanangu hivyo hata wewe pia unatakiwa uvue!”
“No I cant do that!”(Hapana siwezi kufanya hivi) Alikataa Dorothy na Suzanne aliendelea kumshawishi akubali kufanya hivyo lakini bado alikataa.
Dorothy alishuhudia wanaume kwa wanaume wakipapasana, wanawake kwa wanawake wakigusanisha miili yao, alishangaa sana ilikuwa ni mara yake ya kwanza kushuhudia jambo kama hilo likitokea, akiwa mwenye mawazo mengi ghafla alishangaa kumwona mtu aliyehisi kumfahamu, sura ilikuwa ni kama ya kaka yake John akiwa amekumbatiwa na mwanaume mwingine!
“I cant believe this!”(Siwezi kuamini hata kidogo) alisema na kuanza kutembea kuelekea mahali aliposimama kijana yule akiwa amekumbatiwa na mwanaume mwingine. Kweli alikuwa ni kaka yake akiwa amekumbatiwa na mwanaume mrefu mnene.
“Hey John what are you doing here?”(He! John unafanya nini hapa?)
John aligeuka ghafla kuangalia mahali ilipotokea sauti ile, alipogundua alikuwa ni dada yake tena pacha alitoka ghafla katika mikono ya David Syndrome na kuanza kukimbia kwenda nje aibu kubwa ilikuwa imemshika, hakutegemea hata kidogo kama dada yake pia angeweza kuwa pale usiku ule na kugundua tabia yake mpya aliyokuwa amejifunza akiwa Uingereza, yeye na Dorothy walisoma vyuo tofauti.
Suzanne alishuhudia jambo hilo likitokea na kulazimika kumfuata Dorothy kumuuliza kilichotokea na Dorothy hakuwa tayari kujibu kitu chochote aliendelea kumsisitizia Suzanne waondoke.
“Lets go home! I don’t want to stay here anymore!”(Twende nyumbani sitaki kukaa hapa tena)Dorothy alimwambia Suzanne kwa ukatili na bila ubishi Suzanne alianza kuvaa nguo zake na wote wawili waliondoka kurejea nyumbani ikiwa tayari ni saa tisa na nusu za usiku.
Cha kushangaza usiku wa siku hiyo hiyo wakiwa wamelala chumbani, Dorothy aligutuka usingizini na kumkuta Suzanne akiwa amemkumbatia na akimfanyia mambo yasiyostahili na alipojaribu kuhoji Suzanne alilia na kumbembeleza anyamaze na kuvumilia akidai alikuwa katika hali mbaya kimapenzi!
“It is just a massage and nothing more!”(Ninakuchua tu na hakuna kitu kingine zaidi)
“No! No! No!”(Hapana! Hapana! Hapana!)
“I will give you anything you need Dorothy please dont say no!”(Nitakupa kila kitu utakachotaka tafadhali usikatae)
Dorothy alikaa kimya na kumwacha Miss Suzanne afanye kila alichotaka cha ajabu hata yeye alijisikia raha ya ajabu na kujikuta akimkumbatia Suzanne.
Huo ndio ukawa mwanzo wa uhusiano wa kisagaji kati ya watu hawa wawili, Dorothy alizoea mchezo huo kupita kiasi na wakawa kama mtu na mke wake, Suzanne aliyemtunza Dorothy kwa kila kitu na hata alimnunulia gari zuri la kutumia shuleni.
Dorothy na Suzanne walifanya kila walichotaka na Johnson na David Syndrome na walifanya kila walichopenda kuridhishana kimapenzi, kwa David na Suzanne kufanya hivyo kulikuwa ni kujikinga na mdudu waliyemtengeneza bila kujua tayari mdudu alikuwa amerejea kwao.
*****
Miaka miwili baada ya uhusiano huo Johnson alianza kuugua, alivimba matezi yote ya shingoni na akawa anapatwa na homa za mara kwa mara, alipopimwa hospitali alionekana kuwa na kifua kikuu na ikalazimika arudishwe nyumbani Uganda! Majibu hayo yalipomfikia David Syndrome alianguka chini na kupoteza fahamu alipozinduka baadaye alilia akisema.
“It has come back to me!”(Imerudi tena kwangu!
Je nini kitaendelea?
Tukutane Alhamisi mahali hapa

No comments