Header Ads

Kaka amchana Jack Pemba! Adai anafuja pesa wakati hali nyumbani Dar ni mbaya, amefunguka mazito


Stori: Boniphace Ngumije na Andrew Carlos, IJUMAA WIKIENDA
DAR ES SALAAM: Baada ya video ya Mbongo Jack Marshal Pemba anayeishi Uganda kusambaa mitandaoni akiosha gari la kifahari, Range Rover kwa ‘shampeni’ kisha kulifuta kwa dola za Marekani na baadaye kusemekana amewasili nchini, wasomaji walipenda kujua undani wa jamaa huyu na kutafutwa huku kaka yake akisema hali ni mbaya...
 DSC07107
UBUYU ULIKOANZIA
Hivi karibuni kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers kilipokea taarifa kutoka kwa watu wa karibu na pedeshee huyo anayesifika kuwa karibu na bendi nyingi za Bongo kuwa, ana maisha mazuri sana nchini humo na kwamba, mkwanja wake hauna maswali katika matumizi huku wengine wakisema anatanua ‘kufuru’.
“Jack Pemba anatanua kwa kufanya ‘kufuru’, nahisi amepeta mshiko wa maana huko Uganda lakini mkimpata muulizeni anakopatia pesa maana tunasikia anatafutwa mara hivi...lakini nyie OFM mtembeleeni kwao, Tabata-Segerea (Dar), nasikia yupo kwa mapumziko,” kilisema chanzo hicho.
OFM KAZINI
Baada ya ubuyu huo kufika ‘mahali pake’, OFM ilijipanga katika safu na kuanza kumsaka Jack Pemba ikizangatiwa kuwa, licha ya chanzo kusema yupo Tabata, wengine walisema anaishi Gongo la Mboto, wengine Mbezi Beach na wapo waliosema makazi yake ni Masaki, Dar.
DSC07101TABATA YAZAA MAJIBU
Hosana Pemba aliyejitambulisha kuwa ni kaka wa damu wa Jack Pemba ndiye aliyekutwa kwenye nyumba ya Tabata. Kwa hiyo, OFM walioelekea Tabata ndiyo walifanikiwa.
Akijibu swali la kwanza la OFM kuhusu mdogo wake kutua Bongo, Hosana alisema:
“Hapana, hajaja.”
Alipoulizwa mazingira ya maisha nyumbani hapo kwa maana alipo mama mzazi na ndugu wengine, Hosana alisema ni mabaya sana.
KUMBE JAK PEMBA ‘ANAFUNGAGA’ MTAA
OFM ilimuuliza kaka yake huyo kama Jack akitua Bongo huwa anafanya matanuzi hapo nyumbani kwao maana kikipatikana ni lazima kifurahiwe na ndugu ambapo alisema huwanunulia bia watu na kugawa fedha.
“Na siku akiondoka kabisa kurudi huko aliko huwa anamwachia mama shilingi 200,000,” alisema kaka huyo.
KAKA ADAI KULALA CHINI
Kaka huyo ambaye muda mwingi huishi nchini Malawi kutokana na shughuli zake, alisema amejenga nyumba maeneo hayo ili apate sehemu ya kufikia anaporudi Bongo lakini hajaimaliza kutokana na kipato kidogo na anapomuomba Jack amsaidie hatoi  ushirikiano.
ALIPO MAMA WA JACK PEMBA
OFM haikufanikiwa kumpata mama ya Jack Pemba ambaye muda huo.Capture 3
OFM: “Unaweza kunipatia namba za Jack ya huko Uganda aliko?”
Kaka: “Mimi sina namba yake. Kwanza huwa hanipigii simu.”
Hata hivyo, pamoja na kumsubiri sana mama Jack huku mvua ikinyesha lakini hakutokea na haikujulikana alikokwenda.
KABLA YA KUJIKUMBUSHA
Mwishoni mwa mwaka jana, Jack Pemba alisikika kwenye sauti yake aliyoitupia mitandaoni akisema anamiliki magari kadhaa ya kifahari. Aliyataja magari hayo kuwa ni, Range Rover Sports 2016, Alphard, BMW X6, Aud, Hammer H3 na 4matic Mercedes Benz.
CaptureNa akisherehekea bethidei yake kutimiza miaka 42, aliyoifanya Hoteli ya Speke Resort Munyonyo iliyopo kwenye fukwe ya Ziwa Victoria, nje ya mji mkuu wa Uganda, Kampala, Jack Pemba alidaiwa kuteketeza kiasi cha shilingi milioni 100 za Uganda.
TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Jack Pemba ni Mbongo. Alipata umaarufu mwishoni mwa miaka ya 2000 baada ya kutua nchini akitokea Uingereza na kunasa kwa staa wa sinema za Bongo, Aunt Ezekiel lakini baadaye walimwagana. Kule Uingereza inasemekana ana mke Mzungu na watoto.
Jack Pemba pia ni maarufu kwa wanamuziki, hasa Wakongo kwani ni mmoja wa mapedeshee wanaotuza fedha majukwaani huku na yeye akizawadiwa kwa kuimbwa kwenye nyimbo mbalimbali

No comments