Header Ads

Kwa mpango huu, Simba bingwa


KOCHA wa Simba, Jackson Mayanja, hana makeke badala yake amewajenga kisaikolojia wachezaji wake halafu anawapa mazoezi ya nguvu ili kuhakikisha wanashinda mechi zao zote zilizobaki bila kutoa sare hata moja, lengo likiwa ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Hesabu hizo za Mayanja zimekuja huku timu yake ikiwa kileleni mwa ligi hiyo na pointi 57 ikifuatiwa na Yanga yenye 56 na Azam FC yenye 55. Tofauti na Simba na Azam zenye mechi 24, Yanga inazo 23 tu.
Leo Yanga inacheza na Mtibwa Sugar katika ligi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam lakini Simba yenyewe itashuka uwanjani hapo kesho Jumapili kucheza na Toto Africans ya Mwanza.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Mayanja alisema: “Mechi za ligi ndiyo karata yangu ya mwisho kwa kujua mbivu na mbichi, hivyo nawaandaa kisaikolojia wachezaji wangu na kuwapa mazoezi ya nguvu.
“Kwa jinsi tulipofikia, hakuna sare tena katika mechi zilizobakia na tunachoangalia ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo ulio mbele yetu ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri zaidi kwani lolote linaweza kutokea mbele.”
Simba mapema wiki hii ilifungwa na Coastal Union mabao 2-1 katika robo fainali ya Kombe la FA, hivyo msimu huu imebakiza taji moja la kuwania ambalo ni ligi kuu.

No comments