• Latest News

  April 03, 2016

  YANGA YAIPIGA BAO 3-1 KAGERA SUGAR UWANJA WA TAIFA DAR


  GOOOOOO Dk 89, Haji Mwinyi anaunganisha mpira wa kona wa Msuva kwa kichwa na kufunga bao la tatu
  KADI Dk 86, Babu Ally wa Kagera analambwa kadi ya njano kwa kumkanyaga Yondani kwa makusudi
  Dk 83, Mwashiuya tena anaingia vizuri lakini kabla ya mpira haujamfikia Ngoma mabeki Kagera wanaokoa na kuwa wa kurusha

  Dk 81, krosi safi ya MWashiuya lakini Ntala anaokoa na mabeki wake wanaondosha hatari
  SUB Dk 78, anatoka Tambwe, nafasi yake inachukuliwa na Nonga
  Dk 75, krosi safi ya MWashiuya mpira unamfikia Tambwe anapiha kichwa cha kudundisha lakini mpira unatoka nje

  Dk 72, Ngoma anajaribu kwa kupiga shuti kali kabisa, lakini anakuwa hajalenga lango linapaa juuu

  KADI 67 Mwashiuya analambwa kadi ya njano kwa kujiangusha
  Dk 65, JUma Abdul anapiga shuti kali kwelikweli, linagonga mtambaa wa panya na kutoka nje
  GOOOOOO Dk 62, Tambwe anawahadaa mabeki wa Kagera, anaingia ndani ya 18 na kufunga kwa ulainiii baada ya mpira kumtoka kipa na kujaa wavuni
   KADI Dk 61 Haji Mwinyi analambwa kadi ya njano kwa kupandisha daruga

  SUB dk 60, Yanga inamtoa inamtoa Kaseke inamuingiza Gofrey Mwashiuya
  Dk 58, pasi nzuri ya Yondani, lakini Msuva anashindwa kuwa makini na mpira unatoka nje
  KADI Dk 57 Paul Ngalyoma analambwa kadi ya njano kutokana na kuchelewesha muda wakati anatoka
  Dk 53 Telela akiwa amebaki yeye na nyavu anashindwa kulenga lango na mpira unatoka nje

  Dk 52 Kanoni anapiga krosi, hatari kwenye lango la Yanga lakini  mafowadi wanashindwa kuiwahi
  Dk 48 hadi 50, mechi inaonekana upande wa Yanga ambao wamepania kupata bao
  Dk 46 Shabani Ibrahim Chogo analambwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu, anatolewa nje

  DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
  Dk 45, Kanoni analazimika kulala na kuokoa mpira wa Haji Mwinyi, Yanga wanapiga kona lakini dhaifu na kila Ntala ambaye anaonekana kuanza kupoteza muda anaudaka kwa ulaini kabisa.
  Dk 41 hadi 44, mpira unaonekana umepooza zaidi huku kila timu kama imeridhika na sare hiyo katika kipindi cha kwanza

  Dk 38 hadi 40, mabeki wa Kagera wanaonekana kutokuwa makini na kuwapa Yanga nafasi nyingi za kuingia kwenye eneo la penalti. Lakini Yanga pia hawako makini katika suala la umaliziaji
  Dk 37, Ntala anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Tambwe lililokuwa linakwenda langoni na kuwa kona. Inachongwa kona lakini Ntala anaudaka tena kwa ulaini
  Dk 34, Yondani anakwenda kupiga penalti lakini kipa Ntala anaikamata vizuri kabisa

  PENAAAAAT Dk 33, Chogo anamwangusha Ngoma na mwamuzi anasema ni penaat
  Dk 28 hadi 31, zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja huku kila timu ikionekana kucheza kwa kujiamini zaidi

  Dk 27, Kamusoko anapiga mkwaju mzuri wa mpira wa adhabu, lakini unapita juu kidogo ya lango la Kagera

  GOOOOOOO Dk 25, krosi nzuri ya Juma Abdul, Ngoma anaruka na kupiga kichwa safi kabisa, mpira unapita katikati ya miguu ya kipa
  KADI Dk 23, Yondani analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Jumanne, kila timu ina kadi moja ya njano

  Dk 18 hadi 20, Kagera wanaonekana kuimarika na kucheza kwa kujiamini zaidi hali ambayo inawapa Yanga wakati mgumu
  KADI Dk 17 Jumanne anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumkata mtama Tambwe
  Dk 14, Barthez anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Kanoni kupitia mpira wa faulo
  Dk 12, Msuva anapoteza nafasi nyingine tena, krosi nzuri ya Kaseke lakini anashindwa kulenga lango, goal kick

  GOOOOOOOOO Dk 9, Kanoni anapiga krosi nzuri kwa Mbaraka Yusuf naye anaunganisha wavuni kwa mguu wake wa kushoto na kuandika bao la kwanza
  Dk 5, shambulizi kubwa zaidi la kwanza la Yanga, Msuva anaunganisha krosi safi ya mpira wa adhabu wa Juma Abdul, lakini kipa Ntala anaokoa vizuri kabisa
  Dk 3, Ngoma anapiga krosi nzuri inapita mabeki wa Kagera na kumkuta Tambwe lakini anashindwa kuwa mwepesi kuuwahi mpira, kipa Kagera anaudaka kwa urahisi kabisa

  Dk 2, Msuva anaingia vizuri anapiga krosi lakini haimfikii Tambwe aliyemlenga na Kagera wanatoa, inakuwa kona, Yanga wanapiga lakini haina manufaa
  Dk 1, Yanga inakuwa ya kwanza kufika langoni mwa Kagera lakini Ngoma anadhibitiwa vizuri na George Kavila na mpira unaoendeolewa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: YANGA YAIPIGA BAO 3-1 KAGERA SUGAR UWANJA WA TAIFA DAR Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top