Header Ads

Lulu Diva azua timbwili kwenye fumanizi


Video Queen na muigizaji wa filamu anayekuja juu kwa sasa Bongo, Lulu Abasi ‘Lulu Diva’ juzikati alizua timbwili kwenye fumanizi mitaa ya nyumbani kwao, Tandale jijini Dar lililomhusisha shemeji yake, Ijumaa inakuhabarisha.
Ishu ilianza hivi
 


Mapaparazi wetu walienda nyumbani kwa video queen huyo kwa ajili ya mahojiano ya kawaida na mastaa, lakini wakiwa wameshakaribishwa na kuanza maongezi, ghafla aliingia mdada mmoja na kumchukua staa huyo na kuingia naye chumbani kwake. Muda mfupi baadaye walitoka na Lulu Diva aliwaomba radhi waandishi wetu akiaga kuwa ‘anamtoa’ nje mgeni huyo aliyesema ni dada yake.
Achelewa kurejea
 

Wakati mapaparazi wetu wakiwa wanamsubiri na kuona kabisa anachelewa tofauti na ahadi yake, mara akaja jirani yake na kuwajuza kuwa mwenyeji wao alikuwa mtaa wa pili, akiwa ‘amelianzisha’, kwani amemkuta shemeji yake, yaani mwanaume anayeishi na dadake, akiwa ameingiza mchepuko ndani.
“Jamani Lulu Diva huko anabwata balaa, watu wamemzunguka nasikia amefumania, hamna habari nyie? Kama ndugu zake mpo nendeni mkamsaidie,” alisema jirani huyo na kuondoka.


Mapaparazi eneo la tukio
Baada ya kusikia habari hizo, haraka mapaparazi wetu waliibuka mtaa wa pili na kumkuta Lulu Diva akifoka, akimtaka shemeji yake aliyejifungia ndani, atoke nje na mchepuko wake, lakini kwa mshangao wao, wawili hao waliofumaniwa walitokea mlango wa upande wa pili na kutokomea kusikojulikana.

Msikie sasa Lulu Diva
 

“Dah! Ni stori ndefu, huyu aliyefumaniwa ni shemeji yangu, amenishangaza kuleta mwanamke ndani wakati dada yangu kaenda kujifungua, leo karudi ndo tunamkuta shemeji akipikiwa chai tena na mwanamke amevaa mtandio tu, imeniuma ndiyo maana nimezua timbwili huyu mwanamke bado tutamtafuta tu,” alisema Lulu Diva.

No comments