Header Ads

Lulu Diva: Nili-date na mume wa mtu, yakanikuta!


 Video Queen Lulu Abasi ‘Lulu Diva’.

WIKI hii tunaye Video Queen Lulu Abasi ‘Lulu Diva’. Ameonekana kwenye video nyingi ikiwemo ya Mzee Yusuf (Mahaba Niue), Baraka Da Prince (Naogopa) na nyinginezo. Katika maswali 10 aliyoulizwa na mwandishi wetu Hamida Hassan , amefunguka mambo mengi ya kimaisha na kisanii pia. Fuatilia hapa chini… Ijumaa: Uliwahi kuigiza kwenye Igizo la Jumba la Dhahabu, kwa nini uliachana na kazi hiyo na kuamua kuwa Video Queen?

 Lulu Diva: Ni fani iliyokuwa kwenye damu. Napenda sana mambo ya umodo, ndiyo maana nikaja huku nikiamini nitatimiza ndoto zangu. Ijumaa: Mavideo Queen wengi hujikuta wakitembea na wanamuziki ambao wanashiriki kwenye kazi zao, ni kwa nini? Wewe je ulishatoka na mwanamuziki uliyeshiriki kwenye video yake? Lulu Diva: Wapo baadhi wanaofanya hivyo na hiyo si lazima, inategemea na tabia ya mtu. Mimi sijawahi kutembea na mtu niliyefanya kazi yake.
Ijumaa: Kuna madai kuwa wewe ulishawahi kutembea na msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’, unayazungumziaje madai hayo? Lulu Diva: Dah! Watu walihisi tu kwa sababu alikuwa ni mshkaji wangu, sijawahi kutoka naye. Ijumaa: Mavideo Queen wengi mmekuwa mkisumbuliwa na mapedeshee, kwako wewe umewahi kupata usumbufu huo?
Lulu Diva: Ni kweli wanasumbua sana na usipokuwa makini unaweza kujikuta unawapanga.

Ijumaa: Ulishawahi kuwa na uhusiano na mtu mzima ‘shugadadi’ katika mapito yako ya kimapenzi?
Lulu Diva: Ndiyo nilishakuwa naye alinipenda sana, tuliachana kwa sababu mkewe alijua, tukasumbuana sana, yaliyonikuta ni siri yangu.
Ijumaa: Je, mwanaume huyo alikuwa akifanya kazi gani?
Lulu Diva: Dah! Alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa sana hapa Bongo.
Ijumaa: Maisha yako ya kimapenzi kwa sasa yakoje?
Lulu Diva: Niko kwenye uhusiano ambao siyo siriasi sana kwani bado tunachunguzana.
Ijumaa: Wasichana wengi kama wewe wanapenda wanaume wenye pesa, kwa upande wako hilo liko vipi?
 Lulu Diva: Mimi pia napenda mwanaume mwenye pesa kwa sababu kila ninachokifanya kinataka pesa, hivyo nikimpata asiyekuwa na pesa nitamchiti tu.
Ijumaa: Ukiwa na mpenzi wako huwa unapenda kwenda naye wapi?
Lulu Diva: Napenda tujifungie ndani tu, hakuna kwenda popote.
Ijumaa: Pozi gani unalipenda ukiwa naye na ni mavazi gani unapendelea faragha?
Lulu Diva: Napenda anipakate kama mtoto. Kwa upande wa mavazi napenda kuvaa nguo za ndani tu au kanga moja. Ijumaa: Ni mwanamuziki gani unapenda sana kufanya naye video kwa hapa Bongo? Lulu Diva: Nampenda Christian Bella na kuna video nimefanya naye itatoka soon, ni kali sana.

No comments