• Latest News

  April 15, 2016

  Lulu la Diva: Bila mil. 3 hunipati

  Muuza nyago maarufu kwenye video za Kibongo, Lulu Abbas ‘Lulu la Diva’.
  Muuza nyago maarufu kwenye video za Kibongo, Lulu Abbas ‘Lulu la Diva’ amefungukia malipo ya video za Kibongo kuwa amekuwa tofauti na wauza nyago wengine kwani kwake bila shilingi milioni tatu huwezi kumpata. Akichonga na Showbiz Extra, Lulu ambaye yupo kwenye video kadhaa za Kibongo ikiwemo Naogopa ya Mirror na Barakah Da Prince alisema kuwa, wauza nyago wengi wa Kibongo wamekuwa ‘cheap’ sana kwani wapo wanaofanya video hadi bure huku wengine wakilipwa kiduchu. “Mimi sipo kama hao, nipo kazini na malipo yangu ni tofauti hata ukiwauliza hao mastaa wa Bongo Fleva watakwambia, kulipwa kwangu ni kuanzia milioni tatu chini ya hapo wakatambike,” alisema la Diva.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Lulu la Diva: Bila mil. 3 hunipati Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top