Header Ads

Lulu la Diva ‘Mgonjwa’ wa Kioo


    Video Queen, Lulu Abbas ‘Lulu La Diva’ akiwa amejipumzisha ndani kwake.

MAMBO vipi mpenzi msomaji wa Mpaka Home? Spidi yetu ni ileile 120,  tunakupa fursa ya kuweza kujua maisha halisi ya mastaa mbalimbali wakiwa nyumbani.

Leo tunaye Video Queen, Lulu Abbas ‘Lulu La Diva’ anayeishi maeneo ya Magomeni jijini Dar, twende pamoja kujua mengi kutoka kwake:

lulu la diva (3)…Akichoma ubani.

Mpaka Home: Mambo vipi, Lulu mimi nilijua ungeniambia unakaa Masaki kumbe unaishi Magomeni?

Lulu: Hahaa! Unajua siku zote mkataa kwao ni mtumwa. Mimi naishi hapa Magomeni bwana.

Mpaka Home: Kwa uelewa wako, unafikiri nyumba ya staa inatakiwa iweje?

lulu la diva (5)Lulu: Mimi ninafikiria inategemea na uwezo wa mtu kwa kweli lakini japokuwa hata kama huna uwezo wa kukaa nyumba kubwa, unaweza kuitengeza ndani ikaonekana tofauti.

Mpaka Home: Maisha yako ya kawaida yakoje hapa mtaani?

Lulu: Mimi ni mtu wa kawaida sana, ninachojisikia nafanya. Nikitaka kula muhogo kibandani nafanya hivyo sitaki maisha ya kujikweza.

lulu la diva (6)

Mpaka Home: Nimeshangaa sana kukukuta jikoni nilidhani mambo ya moto na wewe ni vitu mbalimbali!

Lulu: Nashukuru kwa kuwa umenikuta mwenyewe maana usingeweza kukubali kama napika, lakini mimi chakula ili nikisikie lazima nikipike mwenyewe kwa mkono wangu.

LULU LA DIVAA (1)

…Akiandaa chakula.

Mpaka Home: Vipi hapa unaishi na shemeji maana huku ndani si mchezo?

Lulu: (Haaah…haa) naishi peke yangu lakini leo yupo mama yangu ni mgonjwa, bado sijaolewa, nikipata mume nitaenda kuishi kwake siyo yeye aje hapa.LULU LA DIVAA (2)


Mpaka Home:
Nini hasa unachokipenda kwenye nyumba yako?

Lulu: Napenda sana usafi. Uchafu ni adui yangu ndiyo maana unaona hapa kila wakati nafukuzana na nzi.

lulu la diva (8)
Mpaka Home:
Ukipata wageni ni kitu gani unapenda kuwaandalia ili kuwafurahisha?

Lulu: Pilau ndiyo chaguo la kwanza maana ni chakula kinachopendwa na watu wengi.

lulu la diva (2)…Akitengeneza nywere

Mpaka Home: Kila mtu ana sehemu yake ambayo anaipenda nyumbani, kwako wewe ni wapi unapopapenda zaidi?

Lulu: Napenda sana kwenye kioo kila mara nikae nikijiangalia basi.

Mpaka Home: Hujawahi kufikiria kuwa na nyumba yako?

lulu la diva (9)…Akila

Lulu: Ndicho kitu kinachoniumiza kila kukicha unajua ukipanga nyumba huwezi kuipamba unavyotaka lakini najua nitafanikiwa maana najipanga kwa ajili ya hilo.

Mpaka Home: Nakushukuru sana Lulu kwa ushirikiano.

Lulu: Karibu tena
.lulu la diva (1)


No comments