Header Ads

Mabasi yaendayo kasi ya Dart Jiji la Dar es Salaam mwisho Mei 2

 Daladala zinazofanya safari zake katikati ya jiji la Dar es Salaam  zimetakiwa  kuondoka   ifikapo Mei 2 Mwaka huu ilikupisha mradi wa mabasi yaendayo kasi kuweza kufanya shughuli zake kuanzia hiyo Mei 10.
 

Juzi, Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene alisema mradi huo utaanza kutoa huduma kwa wakazi wa jiji hilo Mei 10.

Msemaji wa mradi huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar es Salaam (Dacoboa), Sabri Mabrouk alisema wamiliki wote wa daladala walilipwa fidia ya kubadili njia.

“Wamiliki wa mabasi walishalipwa fedha zao tangu Desemba mwaka jana, hakuna anayedai na tumewapa siku saba kuondoka barabarani kabla ya Mei 10,’’ alisema.

Mabasi hayo zaidi ya 30 ya Darts yalianza kupita kwenye njia zote za mradi huo. Changamoto kubwa inayolalamikiwa ni muingiliano wa daladala, magari binafsi, pikipiki na raia kupita bila tahadhari kwenye njia za mradi.

Moja ya mabasi hayo jana lilipata ajali baada ya kukwaruzana na pikipiki eneo la Kinondoni.

“Nasikitika pikipiki zinapita wala madereva hawaangalii, wameshakwaruzana na basi la mradi, sijui itakuwaje mradi utakapoanza, elimu inahitaji kwa wananchi bila hivyo tutawapoteza wengi,” alisema Mabrouk

Alisema wamelazimika kufanya majaribio bila ya kubeba abiria kwa zaidi ya wiki kwa kuwa nauli mwafaka haijajulikana.
1. RUTI YA KIMARA- KIVUKONI  Mabasi Sita (6). Kati ya mabasi Hayo sita wakati wa Kutoka Jangwani matatu yataenda Kimara na Matatu Kivukoni.


2. RUTI YA KIMARA – KARIAKOO Mabasi Sita (6). Kati ya hayo Matatu yataelekea Kariakoo na Matatu Kimara.

3. RUTI YA UBUNGO – KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi Manne yataelekea Ubungo na Manne Kivukoni.

4. RUTI YA UBUNGO – KARIAKOO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi manne Yataenda Ubungo na Manne yataenda Kariakoo.

RUTI YA UBUNGO – MOROCCO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Manne yataenda Ubungo Manne yataenda Morocco.

3X6A3738

6. RUTI YA MOROCCO – KARIAKOO Mabasi sita (6). Kati ya hayo mabasi Matatu Morocco na Matatu Kariakoo.

7. RUTI YA MOROCCO – KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya Hayo Mabasi Manne yataenda Moroco na mabasi manne Kivukoni.

MUDA WA KUONDOKA KITUONI SAA KUMI NA MBILI KAMILI.

1. Kimara Terminal Mabasi Sita (6)

2. Ubungo Terminal Mabasi kumi na mbili (12)


3. Morocco Termial Mabasi kumi na moja (11)

4. Kariakoo Terminal Mabasi kumi (10)

5. Kivukoni Terminal Mabasi kumi na moja (11)

CHANZO: issamichuzi

No comments