Header Ads

Madai ya Diamond kuopoa mpenzi mpya kisha mama yake amfyatukia zari!


 Muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady.

DAR ES SALAAM: Kimenuka tena! Hali ndani ya familia ya staa wa Muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, inadaiwa kuwa si shwari kufuatia mama wa msanii huyo, Sanura Kassim ‘Sandra’ akishirikiana na mwanaye  Esma Platnumz kudaiwa kutibuana na mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ Ijumaa lina ubuyu kamili. 

Chanzo cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina kilidai kuwa, sababu ya kutibuana huko ni baada ya Zari kunasa umbeya kuwa, Esma amemkuwadia Diamond kwa yule video queen aitwaye Irene au Lynn kisha mama Diamond kumkumbatia mrembo huyo na kudai ni mwanaye. 


BOFYA HAPA KUSIKIA CHANZO
 “Ukweli ni kwamba hali si shwari ndani ya familia ya Dangote (Diamond), Zari amemaindi sana kusikia Esma kamuunganishia Diamond kwa yule Lynn (aliyeuza nyago kwenye video ya msanii wa Diamond aitwaye Raymond inayokwenda kwa jina la Kwetu), halafu na mama yake naye anamkumbatia. 

“Kitendo kile kilimfanya Zari ajione kuwa hatakiwi. Kimsingi kilinuka na hata wakati Zari anaondoka kwenda South (Afrika Kusini), hali haikuwa poa. 

MTANDAONI NAKO
 Inaelezwa kuwa, kufuatia kutibuana huko, hivi karibuni Zari alimuunfollow (kumtoa kwenye listi ya watu wake) Esma kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram, jambo
lililoshibisha yale madai kuwa ni kweli kimenuka.


 Aidha, ilidaiwa pia kuwa, kutokana na figisu hizo, Mama Diamond naye aliamua kufuta picha zote za Zari kwenye akaunti yake ya Instagram kuonesha kuwa amemchoka. “Wewe fuatilia huko Insta utaelewa hiki ambacho nakuambia, kwa kifupi ni kwamba Zari, Esma na mama yake ni mvurugano,” kilisisitiza chanzo hicho ambacho kiko karibu na familia hiyo. 

HUYU HAPA MAMA D
 Kufuatia madai hayo, Ijumaa lilifanya jitihada za kumsaka mama Diamond kuzungumzia madai hayo ambapo alipopatikana alimfyatukia Zari kwenye mahojiano ya dakika 45 huku akianika kilicho nyuma ya pazia;

 Ijumaa: Kuna madai kuwa wewe na Zari mmetibuana na kutokana na hilo umefikia hadi hatua ya kufuta picha zake Insta, hilo likoje mama? Mama Diamond: Hayo mambo ya kutibuana yapo tu, siyo kwetu hata kwenye familia nyingine. Ninachojua sasa hivi tuko sawa ila hilo la kufuta picha liko hivi; nimefanya hivyo kwa kuwa nataka nitoke kwenye Insta na sijafuta za Zari tu, nimefuta zote na kubakiza za wajukuu, ya  Diamond na Rommy Jones. 

Ijumaa: Inadaiwa hali si shwari kwenye familia baada ya Diamond kudaiwa kutoka na msichana aitwaye Lynn, mama unasemaje kuhusu hilo? Mama Diamond: Haya matimu kwenye mitandao ndiyo yanazusha mambo ya ajabu, mbona mambo mengine ni ya kawaida kutokea.

 Mimi ni mama hapa nyumbani, hivyo siwezi kumtafutia Diamond mwanamke wala mtu yeyote na msimamo wangu mimi kila aliye kwenye himaya yangu kwangu ni mtoto siwezi kumbagua.

 Swali: Inadaiwa Zari anakuchukia kwa sababu umemkumbatia Lynn na kusema ni mwanao wakati anahisi anatoka na Diamond, hili likoje? Mama Diamond: Sina ugomvi na mtu ila Zari akinichukia, ananichukia mwenyewe, mimi sina tatizo, ujue mimi ni mama maana hata mtu akija kuniuliza eti fulani ana mwanamke nakuwa sijui lolote. 

ESMA NAYE ANENA Kufuatia madai ya kutibuana, Esma naye alipotafutwa alikuwa na haya ya kunena: “Kwenye maisha ya siku zote watu kugombana ni jambo la kawaida. Hata hivyo, nimekuwa nikisikia mara kadhaa watu wakinituhumu kuwa namkuwadia Diamond, mara nimegombana na Zari, hayo ni maneno ya watu tu yanayozushwa kwenye mitandao. 

“Suala la kusema mimi huwa namkuwadia wanawake Diamond, kwanza watu watakuwa wananikosea adabu sana maana Diamond ni mtu mzima na ana maamuzi yake hivyo mimi siwezi kumtafutia demu. “Hilo la kwamba Zari ameni-unfolow kwenye Insta mimi sijui.”

 TUJIKUMBUSHE Mara kwa mara kumekuwa na mvurugano kati ya Zari na mama Diamond akishirikiana na Esma huku utofauti za kimaisha kati Zari aliyezaa mtoto mmoja na Diamond, Latiffah Nasibu ‘Princes Tiffah’ kwani kumekuwa na madai kwamba mama Tiffah amekuwa akitaka kuleta uzungu. 

Mbali na hilo, hivi karibuni kuliibuka madai kwamba, Lynn amekuwa akikumbatiwa na mama Diamond na Esma huku wakidaiwa kujua kuwa ni mchepuko wa Diamond, jambo linalozidi kuchochea fukuto kwenye familia hiyo ambapo Zari anadaiwa kujichimbia Sauz (Afrika Kusini). 
CHANZO: GAZETI LA IJUMAA

UNGANA NASI TWITTER LEO HAPA 2JIACHIETZ

No comments