Header Ads

Madai ya kalio feki la Wema Sepetu, mama yake afunguka..Je anajaladia?


Madai ya staa mkubwa Bongo aliye pia Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu kwamba wowowo lake linazidi kuwa kubwa kwa sababu anatumia dawa za Kichina yanazidi kushika kasi huku kwa mara ya kwanza mama yake mzazi, Mariam Sepetu akifunguka, Amani limechimba ukweli.
MADAI YALIPOANZA
Tangu alipoanza kuongezeka unene miaka ya karibuni, baadhi ya watu, wakiwemo mashoga zake wamekuwa wakimtuhumu Wema kupaka dawa hizo kwa lengo la kutunisha wowowo.

MANENO YAKAHAMIA MITANDAONI
Manenomaneno hayo yakazidi kushika kasi zaidi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kitu ambacho kinadaiwa kuikosesha amani familia ya staa huyo na hata yeye mwenyewe.

PATI YA INSTAGRAM
MWANZA IKAKOLEZA
Kama vile haitoshi, bado siku za hivi karibuni, Wema alitua jijini Mwanza kwa ajili ya shoo ya Pati ya Instagram mjadala huo ukazidi kuwa mkubwa baada ya nyota huyo kutinga ukumbini akiwa amevaa gauni jeupe la kubana na hivyo kumchonga shepu.
Baadhi ya watu walioingia kwenye shughuli hiyo walisema hakuna shaka Wema huyu na yule wa wa enzi za staa wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba ni wawili tofauti.

mamawema1
HATA WALE WA MITANDAONI
Achilia mbali waliozama ukumbini siku hiyo, hata wale walioiona picha yake ya kwenye tukio ilipotupiwa mtandaoni walichangia wakisema Wema anatumia dawa za Kichina kukuza ‘tela’ lake.

WEMA ALIPOTAFUTWA
Jumatatu iliyopita, gazeti hili lilimsaka Wema kwa njia ya simu yake ya mkononi ili kumsomea madai hayo na pia kumsikia anawaambia nini wote wanaomtolea madai hayo, lakini hakupokea.
Ilibidi gazeti ili limtafute kwa njia ya Mtandao wa WhatsApp kwa kutuma ujumbe mfupi huko lakini pia hakujibu licha ya kwamba aliuona na kuusoma.


MAMA YAKE MZAZI SASA
Amani lilimtafuta mama yake aliyemzaa kwa kuamini kwamba, lazima ajue umbo la mwanaye katika kukua kwake na alivyo sasa.
“Nawashangaa wanaomsema vibaya mwanangu kuwa amejaladia (wowowo), wengine wanasema anatumia dawa za Kichani, hakuna ukweli wowote kwani Wema ni mwanangu, namjua alivyo. Hakuna kitu alicho-ongeza kwenye mwili wake.”

WEMA ANA ASILI
YA MKOA WA TABORA
“Mimi ndiyo mama mzazi wa Wema, umbo lake amerithi kutoka mkoa wake (Tabora) alipotoka, hakuna dawa ya Kichina wala ya kabila gani sijui. Wanaosema mwanangu anatumia za Kichinachina  naona wanajisumbua bure.
“Mimi nawajua watu, ni wivu tu hakuna lingine. Tangu kukua kwake Wema umbo lake liko hivyohivyo, wanaosema ni Mchina wameona wampakazie ili aonekane hana uhalisia, sijui wanataka nini? Wameshindwa,” aliwaka mama Wema.

MWAKA JANA
Hata hivyo, mwishoni mwa mwaka jana, Wema aliwahi kumjibu mwandishi wa habari hizi baada ya kumuuliza kuhusu madai ya kutumia dawa za kuongeza kalio ambapo alionesha kusikitishwa na kusema kuwa ni kitu gani atakuwa anakitafuta kwenye mwili wake au uzuri wa aina gani anautaka.
“Siwezi kufanya kitu kama hicho, kwa kitu gani ambacho nakitafuta katika maisha haya mpaka nitumie dawa za kuongeza makalio. Muda huo mimi sina kwa kweli,” alisema Wema.

CHANZO: AMANI

No comments