Header Ads

MADIWANI WA CUF, CHADEMA WASHINDA KESI


Diwani wa Kata ya Manzese (Cuf), Ramadhan Kwangaya akihojiwa na wanahabari nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, Aprili 29, 2016.

Diwani wa Kata ya Gongolamboto, Jacob Kissy akizungumza na wanahabari mara baada ya hukumu kutolewa, nje ya Mahakama ya Kisutu leo.Baadhi ya wafuasi  wao wakiondoka mahakamani hapo baada ya ushindi huo.


MADIWANI wa upinzani kupitia Chama Cha Wananchi (Cuf), Ramadhan Kwangaya (Manzese) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jackob Kissy (Gongolamboto) jijini Dar, leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu wameshinda kesi zilizofunguliwa dhidi yao na waliokuwa wagombea udiwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) za kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo, Kwangaya alisema mpinzani wake alifungua kesi akimtuhumu kwamba katika uchaguzi huo, alifanya fujo katika kituo cha kuhesabia kura, kura zaidi ya elfu moja hazikuhesabiwa na kwamba baadhi ya wasimamizi wa vituo walitumia lugha ya Kiingereza kwa wapiga kura wao.
Kwa upande wa Kissy, aliwaambia waandishi wa habari kwamba amefurahishwa na  maamuzi yaliyotolewa na mahakama na kwamba haki imetendeka. Kesi hizo zilikuwa zikisikilizwa na hakimu wa mahakama hiyo, Lita Tarimo.

No comments