Header Ads

Malaika afungukia kuacha muziki


 Diana Exavery ‘Malaika’.
STAA wa Ngoma ya Zogo, Diana Exavery ‘Malaika’ kwa mara ya kwanza amefungukia ishu inayosambaa kuwa ameachana na muziki kuwa taarifa hizo hazina ukweli na kwamba matatizo aliyonayo ndiyo yamempumzisha kwa muda tu.
Akizungumza na Showbiz Malaika anayebamba na Ngoma ya Zogo alisema kuwa, kutokana na uvimbe uliokuwa ukimsumbua mwilini ulimfanya kupumzika kwa muda hadi atakapofanyiwa upasuaji.
“Nilikuwa nikiteswa na uvimbe uliopo kwenye kizazi na sasa naendelea vizuri. Daktari wangu aliniambia kuwa nipumzike kwa muda wa miezi mitatu na sasa umebaki mmoja hivyo taarifa kwamba nimeacha muziki si za kweli,” alisema Malaika.
Stori na: ANDREW CARLOS/GPL

No comments