Header Ads

Maua Sama afichua la moyoni

MSANII wa muziki wa Sweet Reggae, Maua Sama amefunguka kuwa siri kubwa ya kuanza kutoka na kujulikana ni ujasiri wake na kudai kuwa kinyume na hapo basi angekuwa ni mfanyakazi wa benki na siyo mwanamuziki.

Maua, staa wa wimbo wa Mahaba Niue, amesema kuwa muziki ulimkatisha tamaa wakati akitafuta njia ya kutoka kisanii na kuwa alishaanza kufikiria akafanye kazi benki au awe mjasiriamali.

“Nilikuwa sipati sapoti ya kutosha, sikusogea, nikakata tamaa, nikafikiria bora nikasome niwe ‘banker’ au mjasiriamali lakini nafsi ikaniambia niendelee kupambana. Namshukuru Mungu leo hii nimeanza kupata mafanikio, naungwa mkono na mashabiki na ninashukuru kwa sapoti yao, nakuwa na furaha sana,” alisema Maua.

No comments