Header Ads

Mauno ya Snura yamdatisha staa wa muziki kutoka Nigeria, Don JazzyMAUNO ya mkali anayekimbiza kunako Muziki wa Mduara, Snura Mushi ‘Snura’ yameonekana kumdatisha staa wa muziki kutoka Nigeria, Don Jazzy kufikia hatua ya kuipongeza video ya bishosti huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Mavins-Boss-Don-Jazzy-Threw-A-Light-Shade-At-Linda-IkejiDon Jazzy
Akichonga na Showbiz Xtra, Snura alisema alipata taarifa juu ya Don kudatishwa na video hiyo iliyojaa mauno na kwamba ni jibu kwa wanaoona muziki anaofanya hauendani na maadili.
“Kawaida ya Watanzania ni kusifia visivyo vyao na kuponda vitu vya kwao. Sasa hilo ni tatizo maana wageni wanakubali mambo tunayoyafanya. Mtu kama Don ambaye sina ukaribu naye kusifia video yangu ni jambo kubwa,” alisema Snura.

No comments