Header Ads

Meya jiji la Dar aibua sakata la UDA


MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amemuomba, Rais John Magufuli, kumulika uozo uliopo ndani ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), ili lirudishwe mikononi mwa jiji hilo.

ISAYA MWITA.
Akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwita alidai mchakato wa uuzaji wa shirika hilo haukuwa halali kutokana na ukiukwaji wa kanuni na taratibu za uuzwaji wake uliofanywa na uongozi wa jiji uliomaliza muda wake.
Alisema ni vyema shirika hilo likarudishwa mikononi mwa jiji ili kuokoa fedha za wananchi zinazopotea katika shirika hilo.


Kwa upande wake, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, ambaye alialikwa na Meya huyo kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo kama Mjumbe wa Baraza la Madiwani la Jiji pamoja na 


Mbunge wa Kawe Halima Mdee, alisema katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika juzi ambacho kilimshilikisha Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, kiliamuakuandika barua kwenda kwa Msajili wa Hazina ya kutokutambua umiliki huo wa UDA na kwamba hata kama kuna hisa ambazo zimewekezwa na mali nyingine hazitarudishwa na badala yake zitazuiwa mpaka pale watakapofanya hesabu kufahamu mali kamili za shirika hilo.

Alidai hata baadhi ya nyaraka ambazo zilitoka kwa Msajili wa Hazina kwenda kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilionyesha kwamba taratibu za uuzwaji wa shirika hilo hazikufuatwa.


“Na zipo baadhi ya nyaraka zinaonyesha kuwa wapo vigogo wengi ambao wako nyuma ya shirika hilo, lakini kamati za jiji ambazo zimeundwa kuchunguza ripoti hizo zitatoa taarifa kamili,” alisema.


Kwa upande wake, Mdee alisema wanashangazwa na kitendo cha Waziri wa Nchi, Ofisi, ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene, kutangaza kuvunja Machinga Complex bila kushilikisha uongozi wa jiji.


Alisema kisheria jiji ndilo lenye mamlaka ya mali yoyote katika jiji, hivyo kunapotokea jambo lolote kuhusiana na mali ya jiji ni lazima mhusika ajulishwe.
Alitoa rai kwa mkuu wa mkoa kushirikiana na uongozi wa jiji katika kufanya kazi endapo anahitaji afanikiwe katika kuliendeleza jiji hilo, huku Meya wa jiji Mwita akisema yuko tayari kufanya kazi na mkuu huyo wa mkoa endapo atahitaji.
CREDIT; NIPASHE

No comments