Header Ads

Miss Dar City Centre 2016 kuzinduliwa Jumamosi hii

Aliyekuwa mshindi wa Miss Dar City Centre 2014, Jihan Dimechk.

SHINDANO la kusaka warembo lijulikanalo kama Miss Dar City Centre linatarajiwa kuzinduliwa rasmi Jumamosi hii, Aprili 23 ndani ya Ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko mratibu wa shindano hilo, Nancy Joseph alisema ufunguzi huo ni maalum kwa ajili ya kuelekea katika shindano lenyewe litakalofanyika Mei 21, mwaka huu.
“Tutakuwa na wadau na wakurugenzi mbalimbali wa masuala ya urembo na lengo kuu ni kulizindua rasmi shindano hili,” alisema Nancy.
Mara ya mwisho kufanyika shindano la Miss Dar City Centre ilikuwa mwaka 2014 ambapo Jihan Dimechk aliibuka kidedea.Shindano hili limedhaminiwa na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers.

CHANZO:  Andrew Carlos,RISASI mchanganyiko

No comments