Header Ads

MISS DAR CITY CENTRE WAFANYA USAFI KUMUUNGA MAKONDAWASHIRIKI wa shindano la kusaka warembo lijulikanalo kama Zan Aqua Miss Dar City Centre 2016, leo wamefanya usafi katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam kama sehemu ya kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar,Paul Makonda katika kampeni ya usafi wa jijini hapa.
Mamiss hao wamefanya usafi katika maeneo ya Magomeni jijini Dar na baada ya kumalizika usafi huo walielekea katika Viwanja vya Leaders Club ambapo Makonda alizindua rasmi kampeni ya kufanya usafi katika maeneo ya jiji na kila siku ya Jumamosi wananchi wote kuhakikisha hawafungui maduka yao hadi majira ya saa tatu asubuhi.
 

Katika kufanya huko usafi, Mamis hao zaidi ya kumi walikuwa wamevalia tisheti za shindano la Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Global Publishers wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Risasi, Championi, Amani pamoja na Ijumaa Wikienda.
 

Shindano hilo la Zan Aqua Miss Dar City Centre linatarajiwa kufanyika Mei 21, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Golden Tulip City Centre. Wadhamini wa shindano hilo ni Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba, Golden Tulip Dar City Centre, TV1, Zan Aqua (Maji ya kunywa), M&J Printing pamoja na Super Model Collections.

No comments