• Latest News

  April 21, 2016

  Naibu Meya wa Jiji La Dar es Salaam Kupatikana Leo


  Meya wa jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita
   
  Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, anatarajiwa kupatikana leo katika kikao cha kwanza cha Baraza la Jiji kitakachofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee.

  Uchaguzi wa naibu meya unafanyika baada ya kukamilika kwa mchakato wa kumpata meya wa jiji hilo uliohitimishwa Machi 22, mwaka huu kufuatia kutawaliwa na ‘figisufigisu’ kati ya CCM na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) zilizosababisha uaharishwe mara tatu.

  Katika kinya’nga’nyiro hicho, Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema), Isaya Mwita aliibuka kidedea kwa kupata kura 84 dhidi ya Diwani wa Kata ya Mburahati (CCM), Yusuph Yenga aliyepata kura 67.

  Meya wa jiji hilo, Isaya Mwita jana alisema  kuwa, maandalizi ya kikao hicho kitakachokuwa na ajenda ya uchaguzi wa kumpata naibu meya yamekamilika.

  Wagombea nafasi hiyo ni Kafana Mussa wa (CUF) na Mariam Lulida wa CCM.

  Tofauti na uchaguzi wa meya, uchaguzi wa leo hautarajiwi kuwa na mvutano mkubwa baina ya Ukawa na CCM kwa kuwa haujumuishi madiwani wote wa jiji hilo, isipokuwa kitakuwa na wajumbe 18.

  Kati ya wajumbe hao, kila manispaa itatoa wajumbe wanne wakiwamo mameya, wakati wabunge watano wa majimbo wataruhusiwa kuingia kwenye baraza hilo litakalokuwa chini ya uongozi wa meya huyo mpya. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Naibu Meya wa Jiji La Dar es Salaam Kupatikana Leo Rating: 5 Reviewed By: 2jiachie
  Scroll to Top