Header Ads

NAY WA MITEGO ANASA PENZI LULU

 MAHABA niue! Hiyo ndiyo kauli nzuri unayoweza kuitumia kuelezea uhusiano wa kimapenzi unaoendelea kati ya staa wa Ngoma ya Shika Adabu Yako, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na ‘video queen’ anayekuja kwa kasi, Lulu Abbasi ‘Lulu Ladiva’. 

 ‘Video queen’ anayekuja kwa kasi, Lulu Abbasi ‘Lulu Ladiva’.
Madai ya kwamba wawili hao ni wapenzi, yaliwasilishwa kwenye dawati la gazeti hili na chanzo chetu ili kupata ukweli, Ijumaa liliingia mzigoni. Wa kwanza kupatikana alikuwa ni Lulu Ladiva ambapo alikiri kuwa in love na mwanamuziki huyo, akafunguka: “Kweli kabisa nipo ‘in love’ na Nay wa Mitego, tena sasa ni muda mrefu tumekuwa wote sema mwanzo hatukupenda kuweka penzi letu hadharani, najivunia kuwa na Nay kwa kuwa ananiheshimu na kunijali japo migongano kwenye uhusiano huwa haikosi, mimi nipo tayari kumvumilia kwa namna yoyote ile kwani moyo wangu umeshapenda na sioni kitu cha kututenganisha tena.” Kwa upande wake Nay alisema: “Lulu Ladiva kwa sasa ndiye usingizi wangu sema mmechelewa kujua, mbona kitambo tu nipo naye maana tangu nimeachana na Shamsa huyu ndiye demu aliyeshikilia mikoba yake.”

No comments