Header Ads

Nimubona: Kessy hanizidi kiwango, bahati tu

 Beki wa kulia wa Simba, Mrundi, Emery Nimubona.
ANACHOONGAA! Baada ya kuhakikishiwa kucheza mechi zote kuziba pengo la Ramadhan Kessy, beki wa kulia wa Simba, Mrundi, Emery Nimubona, amesema namba hiyo ilikuwa yake tangu zamani, lakini Kessy akapata bahati tu kuwa chaguo la kwanza.
Nimubona aliyesaini miaka miwili Msimbazi mwanzoni mwa msimu huu, amekuwa chaguo la pili mbele ya Kessy lakini sasa ana uhakika wa kucheza katika mechi tano za ligi kuu walizobakiza kufuatia Kessy kufungiwa mechi tano kwa kosa la kumchezea rafu mbaya fowadi wa Toto, Edward Christopher.
Akizungumza na Championi Jumatano, Nimubona alisema Kessy hakupewa kipaumbele kwa kumzidi kiwango, bali alipata bahati ya kupendwa na kocha.
“Sisemi kama ni mbaya, ila siamini kama Kessy kiwango chake kinazidiana na changu. Chochote anachokifanya nakifanya, sioni ni kitu gani naweza kujifunza kwake, maana tunalingana viwango, sema tu ni bahati tu ya kupangwa na kocha,” alisema beki huyo anayehimili pia kiungo wa kulia.


No comments