Header Ads

Padri amtolea tamko Jokate Chanzo Ali Kiba


 Mbongo Fleva na Miss Tanzania No. 2, 2006, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Baadhi ya watu waliodai kuwa wao ni waumini wa Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay jijini Dar es Salaam ambako anaabudu Mbongo Fleva na Miss Tanzania No. 2, 2006, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ wamesema nyota huyo hatakiwi kushiriki ibada kwa vile uhusiano wake na Mbongo Fleva, Ali Kiba upo wazi sana, sasa kanisa hilo limetoa tamko.

Akizungumza juzi kanisani hapo, padri aliyejitambulisha kwa jina moja la Edward ‘Faza Edward’ alisema wao kama kanisa wanamtambua Jokate kama muumini wao wa miaka mingi na kwamba mambo mengine hayawahusu.
“Jokate namtambua kama muumini wetu hapa ana anashiriki vizuri tu. Sisi hatuna tatizo naye. Kwanza sisi  mtu yeyote anaruhusiwa kuja kusali hapa, hata kama ni Mwislam ilimradi tu afuate taratibu zetu.
“Kwa hiyo Jokate tunaye hapa kanisani na anaendelea vizuri tu. Umemuulizia na paroko, yeye muda huu ana wageni,” alisema Faza Edward.

Awali waumini hao walisema kuwa, kitendo cha Jokate kuonekana kwenye vyombo mbalimbali vya habari akiwa na Kiba huku si mwanandoa wake jambo ambalo wao wanaliona si sawasawa kwa vile mrembo huyo hushiriki pia kuimba kwaya ya kanisa hilo.

Mwaka jana, gazeti dada na hili, Ijumaa liliandika habari yenye kichwa kisemacho; Waumini: Jokate anatutia aibu.
Katika habari hiyo, Jokate alidaiwa kuwakera waumini wenzake kufuatia kupiga picha za nusu utupu na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii huku midume ikijirushia na kujifaidia kwa macho.
Pia, alilalamikiwa kwa tabia yake ya kupanda jukwani kwenye kumbi za muziki na kunengua huku yeye akiwa ni mwanakwaya wa kanisa hiyo.

Akijitetea kuhusu madai ya waumini wenzake katika habari hiyo, Jokate alisema kuwa, kanisa hilo halimzuii kuvaa nguo fupi wala kukata mauno jukwaani kama mwanamuziki kwani kazi ni kazi.
Alisema kanisani anakwenda kama kawaida na kwaya anaimba kama ‘kawa’.
Katika habari hii mpya, Jokaye alipoulizwa alisema: “Mimi sitaki mnifuatilie mambo yangu ya imani, sitaki kabisa, mnanikwaza.”

Waandishi Hamida Hassan na Imelda Mtema/GPL

No comments