Header Ads

PAPA WEMBA AMELISHWA SUMU?


BADO kifo cha Mwanamuziki wa Dansi na Rhumba, Shungu Wembadio ‘Papa Wemba’ kinazidi kuzua maswali mengi huku watu mbalimbali wakijenga hoja kuwa huenda mwanamuziki huyo mwenye heshima Afrika aliwekewa sumu kwenye moja ya maiki alizotumia wakati akitumbuiza tamashani huko Ivory Coast.
Hoja hiyo inayosapotiwa pia na Mtandao wa Kinshasa-makomba.com imeibuka kufuatia video iliyosambaa mitandaoni inayomuonesha mwanaume mmoja mrefu, mweusi akipanda jukwaani kisha kuchukua moja ya maiki alizokuwa anazitumia Papa Wemba na kwenda nayo kusikojulikana.
Aliirudisha muda mchache baadaye na Papa Wemba alipoitumia tu ndipo alidondoka chini na kupoteza maisha usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita.
Hata hivyo, taarifa za awali zilidai mwanamuziki huyo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa shambulio la moyo lakini kutokana na video hiyo huenda taarifa nyingine ikaibuka.

No comments