Header Ads

Yanga wawasili, wachekelea agizo la Serikali..Ni lile la kuitisha uchaguzi mkuu ulioshindwa kufanyika kwa muda mrefu...


WAKATI Yanga ikitua nchini jana mchana kutoka nchini Misri ilikokwenda kwa ajili ya mechi ya marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly na kufungwa mabao 2-1, wanachama wa klabu hiyo wamechekelea agizo la serikali la kuwataka kufanya uchaguzi mkuu kabla ya Juni 30 mwaka huu.

Mabingwa hao wa Bara walitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa saba mchana na kulakiwa na mashabiki kadhaa wa klabu hiyo wakiogozwa na kikundi cha ngoma.
Yanga imetupwa nje ya michuano baada ya kufungwa jumla ya mabao 3-2, baada ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa zaidi ya wiki mbili zilizopita na sasa itashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho.
Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti jana, wanachama hao wamesema kukaa kwao bila kufanya uchaguzi muda mrefu ilikuwa ni kuvunja katiba na wanashangaa serikali na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) nao kuwa kimya.
Mmoja wa wanachama hao (jina tunalihifadhi) aliliambia gazeti hili jana kuwa wako tayari kufanya uchaguzi mkuu na wamefurahi kupata mwongozi wa serikali kuwa katiba itakayotumika kwenye uchaguzi huo ni ile ya mwaka 2010 na si iliyofanyiwa marekebisho katika mkutano mkuu wa wanachama wa 2014.
Alisema katiba hiyo ndiyo halali na itakayotoa nafasi kwa wanachama kuchagua viongozi watakaowaongoza na siyo inayompa madaraka mwenyekiti kuteua wjumbe wa kamati ya utendaji anaowataka.
"Katiba ya 2010 ndiyo halali, ilimuingiza madarakani Madega (Imani), Nchunga (Lloyd) na uongozi wa sasa, ukweli ni kwamba wanachama tumechoka na sasa tunahitaji kufanya uchaguzi," alisema mwanachama huyo mkongwe.
Kiongozi mmoja wa kamati ya utendaji (jina tunalihifadhi), ambaye anaungwa na kundi kubwa la wanachama alisema mwongozo wa kutumia kadi za zamani utasaidia uchaguzi huo kushirikisha wanachama wenye mapenzi ya 'dhati' na klabu hiyo kwa sababu utaratibu kutoa kadi mpya haukufuata vigezo vya kupata uanachama.
"Kadi halali ya Yanga lazima iwe na sahihi ya mwenyekiti kama ilivyoelekezwa kwenye katiba , zile kadi za benki ya Posta ni za kibiashara na hazina saini ya mwenyekiti na zimekuwa zikitolewa pale Kwa Chichi (baa iliyoko jirani na Uwanja wa Uhuru), ni rahisi hata mashabiki wa Simba kuzipata na kutuingizia 'virusi' klabuni kwetu," alisema kiongozi huyo.
Aidha, manachama mwingine wa klabu hiyo (jina linahifadhiwa), alisema anataka kuona uchaguzi unafanyika kwa sababu viongozi walioko madarakani wameshindwa kujenga hata uzio wa Uwanja wa Kaunda kwa muda wote waliokuwa madarakani.
"Aende tu, miaka nane ya kukaa Yanga amekuwa ni mtu wa ahadi na kutueleza mipango 'hewa', ameshindwa hata kutujengea ukuta, tulibweteka sana kwa kumtarajia atatufanyia mazuri," alisema mwanachama mwingine.
Aliongeza wanachama wa Yanga wawe makini katika kuchagua viongozi ili makosa yaliyojitokeza katika uongozi uliomaliza muda wake yasijirudie tena kwenye klabu yao.
Baraza la Michezo Tanzania (BMT) lilitangaza kuwatambua viongozi wa klabu tatu kati ya 16 tu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara, ambazo ni Simba ya Coastal Union na African Sports.
Yanga (1)
Yanga (2)
Yanga (3)
Yanga (4)
Yanga (5)
Yanga (6)
Yanga (7)
Yanga (8)
Yanga (9)
Yanga (10)
Yanga (11)
Yanga (12)
Yanga (13)
Yanga (14)
Yanga (15)
Yanga (16)
Yanga (17)
Yanga (18)
Yanga (19)
Yanga (20)
Yanga (21)
Yanga (22)
Yanga (23)
Yanga (24)
PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL

No comments